Muonekano wa eneo linaloandaliwa kujenga njia ya reli kwa ajili ya kusafirisha mizigo inayoingia na kutoka bandari kavu, Kwala mkoani Pwani wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo.

UJENZI WA BANDARI KAVU, KWALA VIGWAZA: NAIBU WAZIRI NDITIYE AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa bandari kavu, Kwala kuhusu eneo la njia ya reli itakayoingia bandarini humo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bandari hiyo mkoani Pwani. Wa kwanza kulia Kaimu Meneja wa Badari ya Dar es Salaam, Fred Liundi na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Mhandisi Charles Ogare.
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO AKIPATA MAELEKEZO
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyesimama katikati) akipata maelezo kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa bandari kavu, Kwala mkoani Pwani kutoka kwa Mkurugenzi wa huduma za Uhandisi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mhandisi Charles Ogare (anayetoa maelezo). Wa kwanza kulia ni Meneja wa Mradi huo kutoka SUMA JKT, Raymond Kweka.
NAIBU WAZIRI AKIPATA MAELEKEZO
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akipitia ramani ya mpangilio wa matumizi ya eneo la bandari kavu, Kwala mkoani Pwani wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bandari hiyo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mhandisi Charles Ogare.
Ad

Unaweza kuangalia pia

“Nani aliyeunda Jumuiya ya Madola na kwa nini?”

Malkia Elizabeth II pamoja na mawaziri wake wakuu wa Jumuiya ya Madola mwaka 1962. Picha: …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.