Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu

MAONESHO HAYA NI FURSA MUHIMU KWA WAJASIRIAMALI – Dkt. TIZEBA

Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba amewataka wajasiriamali kote nchini kuchangamkia fursa ya kutembelea katika Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba
Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba akizungumza jambo mara baada ya kuwasili kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

Katika maonesho hayo ambayo yalianza Oktoba 23 mwaka huu, Dkt Tizeba amesema kuwa hiyo ni fursa kwa wananchi kuweza kujielimisha katika maeneo mbalimbali ya teknolojia za viwanda hususani viwanda vidogo, lakini pia wajasiriamali kupata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wenzao wa maeneo mengine nchini na nje ya nchi.

Ad

“Nitoe wito kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu na mikoa ya jirani kama Mara, Mwanza na Shinyanga wajitokeza  kwa wingi kushiriki maonesho haya maana hii ni fursa muhimu kwao katika kuakisi kwa vitendo Tanzania ya viwanda” Alisema Dkt Tizeba

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb)
Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza jambo wakati akikagua mashine zinazotengenezwa na SIDO TDC kwa ajili ya uchakataji wa mazao mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu

Dkt Tizeba amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka kwa kubuni jambo hilo sambamba na kumpongeza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage kwa kuwaalika wajasiriamali, na wataalamu waoneshaji wa teknolojia mbalimbali kwani jambo hilo litatoa fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na mikoa mingine kuona ushindani katika uongezaji wa thamani wa mazao mbalimbali na fursa kwa wajasiriamali kujifunza kutoka kwa wenzao.

Aidha, Dkt Tizeba amesema kuwa Maonesho hayo ya SIDO ambayo ni ya kwanza kufanyika Kitaifa yatawasaidia wajasiriamali kote nchini kupanua masoko ya bidhaa zao.

Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO) yakiwa na Kauli Mbiu isemayo PAMOJA TUJENGE VIWANDA KUFIKIA UCHUMI WA KATI”. yalifunguliwa rasmi na Waziro Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa siku ya Jumanne Oktoba 23, 2018 na yanatarajiwa kuhitimishwa siku ya Jumapili Oktoba 28, 2018.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Je! Wajua Mchango wa Madini ya Tanzanite katika Pato la Taifa?

Madini ya Tanzanite, yanayopatikana pekee katika eneo dogo la Mererani, Tanzania, ni miongoni mwa rasilimali …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *