MAKAMU WA RAIS AKATAA KUZINDUA STENDI YA MAILI MOJA KIBAHA

MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua stendi mpya ya mabasi Kibaha .
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekataa kuzindua stendi kuu mpya ya Mailimoja Kibaha mkoani Pwani, akiwa katika ziara yake mkoani humo.
Hatua hiyo ameifikia kutokana na kupata wasiwasi wa utekelezaji wa mradi kuwa na baadhi ya mapungufu ambapo amedai baada ya kufanya uchunguzi wiki mbili ama tatu zijazo atakwenda kuuzindua.
Akizungumza katika stand hiyo, Samia alieleza, kuna minong’ono wameisikia kuhusu mradi huo hivyo ni jukumu lake kuibeba na atakapo jiridhisha atarudi kwa mara nyingine .
Hata hivyo, amesema atakutana na mkuu wa wilaya, mkurugenzi na mkuu wa mkoa kuzungumzia suala hilo. “Msishtuke kwa hili ni kawaida kwa kuchukua hatua za aina hii ili kujiridhisha kwa maslahi ya halmashauri, mkoa na watumiaji kijumla “Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni sikivu na kusikia malalamiko ya wananchi, tumepata malalamiko kidogo kuhusu stand hii, serikali ni ya uwazi na ukweli hivyo sitofungua stendi “alisisitiza Samia.
MAKAMU WA RAIS AKIPATA MAELEKEZO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uzalishaji Mhandisi Farid M. Abdallah wakati akikagua shughuli za ujanzi wa Reli ya Kisasa “Standard Gauge” katika kijiji cha Soga wilyani Kibaha mkoani Pwani.
Samia alimpongeza mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha, Jennifer Omolo na mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama na wahusika waliohusika kufanikisha mradi huo. Nae waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa -TAMISEMI ,Selemani Jafo alisema yeye kama waziri wapo wataalamu wanaohakiki lakini ameridhishwa na kazi hiyo .
“Kwani kila kazi ina changamoto za kibinadamu, hasi na chanya, lakini wamejitahidi “alisema Jafo. Jafo alieleza, mradi huo umepata msaada wa mkopo nafuu kutoka bank ya Dunia ambao wamepata fedha za kimarekani dollar milioni 255 .# Alielezea , wanagusa miji 18 na wanachokifanya wanagusa stendi tisa, barabara za miji kwa kiwango cha lami na madaraja makubwa ya kisasa.
Wakitoa kero ya stand hiyo, madereva pikipiki walidai eneo lililotengwa kwa ajili yao halina sehemu ya kujikinga hivyo kusababisha usumbufu wakati wa mvua na jua. Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha, Jennifer Omolo alisema katika stendi ndogo ya awali walikuwa wakikusanya ushuru sh. 950.000 kwa siku ambapo sasa wanakusanya sh. milioni 1.6 .Alisema mradi huo umegharimu sh. bilioni 2.9 na walishamlipa mkandarasi bilioni 2.7 ,stendi hiyo itakuwa na mabanda kumi ya kukatia tiketi, mawakala 40 ,eneo la tax, na wafanyabiashara ndogondogo wanaojiingizia kipato kwa kuuza biashara zao wapo 100 .
Samia akiwa katika ziara yake Kibaha vijijini na mjini pia alipata fursa ya kutembelea mradi wa reli ya kisasa ya standard gauge kujionea namna unavyoendelea.
Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *