Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akifungua mkutano wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Mipango Miji, wengine kulia ni Msajili wa Bodi Hellen Mtutwa na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi Profesa Wilbert Kombe unaofanyika katika jiji la Dodoma jana.

MARUFUKU KUPIMA MASHAMBA BILA KUPANGWA – WAZIRI LUKUVI

Serikali imezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatoa vibali vya ujenzi wa nyumba ndani ya siku tatu na kazi hiyo isimamiwe na Maofisa Mipango Miji.

Aidha, imesisitiza kuwa zoezi la urasimishaji katika maeneo yaliyojengwa nyumba kiholela lazima yarasimishwe na zoezi hilo halitakiwi kubomoa nyumba ya mtu yoyote.

Ad

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi wakati akifungua mkutano wa tano wa Bodi ya Wataalamu wa Usajili Mipango Miji unaoendeleo katika jiji la Dodoma.

Baadhi ya wajumbe wakifatilia mkutano
Baadhi ya Wataalamu wa Mipango Miji wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa tano wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji unaofanyika katika jiji la Dodoma.

Lukuvi alisema vibali vya ujenzi wa nyumba katika maeneo mbalimbali lazima vitolewe aidha katika eneo lililopangwa ama lisilo pangwa na cha msingi serikali inachotaka ni kuwa na majengo yaliyo katika mpangilio mzuri na kuongeza kuwa ucheleweshwaji wowote utoaji kibali lazima mhusika afahamishwe sababu za kucheleweshewa kupatiwa kibali.

Kwa mujibu wa Lukuvi lengo la Maofisa Mipango Miji kupewa mamlaka ya kutoa vibali vya ujenzi badala ya wakuu wa idara wa halmashauri husika linatokana na baadhi yake kuongozwa na watu wasiokuwa na taaluma za mipango miji jambo linaloweza kuvuruga upangaji miji bora kwenye maeneo.

Pia ametaka nakala za vibali vya ujenzi vitakavyotolewa na kuhakikisha nakala hizo za vibali zinaenda pia katika ofisi za maafisa watendaji wa mitaa kwa kuwa watendaji hao wanapaswa kufahamu ujenzi unaoendelea katika maeneo yao.

Kikao cha wataalamu Miapango Miji
Baadhi ya Wataalamu wa Mipango Miji wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa tano wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji unaofanyika katika jiji la Dodoma.

Lukuvi ameitaka Bodi ya Usajili Mipango Miji kuandaa muongozo utakaosaidia watendaji wa mitaa kuwa na ufahamu katika kusimamia mipango ya uendelezaji miji jambo litakalosaidia pia kuepuka   ujenzi holela katika baadhi ya maeneo.

Akigeukia suala la urasimishaji maeneo yasiyopimwa, Lukuvi alisema pamoja na zoezi hilo kufanyika nchi nzima lakini hakuna nyumba itakayovunjwa katika zoezi hilo na kutaka makampuni yote yatakayotaka kufanya kazi ya urasimishaji kutuma maombi yao kupitia ofisi za wilaya na kuacha kuenda moja kwa moja kufanya kazi hiyo kupitia kamati maalum za maeneo husika na kusisitiza kuwa zoezi hilo lazima liratibiwe na Maofisa Mipango Miji.

Katika hatua nyingine, Lukuvi amepiga marufuku upimaji mashamba katika maeneo mbalimbali bila ya kupangwa na kubainisha kuwa serikali haitakubali kadhia hiyo iendelee kushamiri kwani suala hilo linafanya miji kukosa maeneo ya wazi, mashule, masoko na hospitali.

Wajumbe wakifatilia mkutano
Baadhi ya Wataalamu wa Mipango Miji wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa tano wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji unaofanyika katika jiji la Dodoma.

Salfonce Kesi Mtafiti na mwalimu katika Chuo cha Ardhi alisema, kwa sasa mambo mengi ya upangaji miji katika maeneo mbalimbali nchini hayaendi vizuri kutokana na mipango kufanywa na watu wasio na taaluma ya mipango miji.

Alisema, ni lazima suala la mipango miji katika maeneo lianze ndipo mipango mingine ya maendeleo iendelee kama vile huduma za maji, barabara pamoja na huduma nyingine za jamii.

Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili Mipango Miji Profesa Wilbert Kombe alisema bodi yake imeanza kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha taaluma ya Mipango Miji inakuwa na wataalamu wanaozingatia sheria na kuchangia kuwepo miji bora na iliyopangika na kubainisha kuwa mahali popote sura ya miji ndiyo inayotoa taswira ya maisha ya eneo husika.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *