TANZANIA YARIDHIA AfDB KUONGEZEWA MTAJI

  • Tanzania imeunga mkono uamuzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB wa kutaka kuongezewa mtaji ili iweze kutekeleza majukumu yake ya kutoa mikopo kwa nchi wanachama wa benki hiyo kwa lengo la kuchochea zaidi maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
  • Akizungumza baada ya kumalizika kwa mkutano wa 7 wa magavana wa ambao ni Mawaziri wa Fedha kutoka nchi 54  wanachama wa Benki hiyo, Mjini Washington DC, Marekani, Waziri wa Fedfha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ameeleza kuwa AfDB imefanya mambo makubwa nchini Tanzania ndio sababu inaunga mkono kusudio hilo.
  • Amesema kuwa Benki hiyo imeipatia Tanzania mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, kilimo, nishati na maji.
  • Benki inataka kuongezewa mtaji kwa asilimia 200 kutoka wastani wa UA bilioni 67.69 hadi UA 191.89 (kutoka dola za Marekani 94.76 hadi dola bilioni 268.6 ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na kijamii ya nchi wanachama hususan katika ujenzi wa reli, barabara, usafiri wa anga, tehama, bandari, uzalishaji na usambazaji wa nishati.
  • “Wakati umefika ili twende haraka zaidi, mitaji sehemu nyingine imepungua, pendekezo la kuongeza mtaji wa benki hii ni jema na matokeo ya miradi inayofadhiliwa na Benki hii yanaonekana katika nchi zetu za kiafrika kwa sababu benki hii iko Afrika na inaijua Afrika tofauti na benki nyingine” alisisitiza Dkt. Mpango
  • Uamuzi wa nchi za Kiafrika zenye hisa katika Benki ya Maendeleo ya Afrika ya kutaka Benki hiyo iongezewe mtaji ulitolewa wakati wa mkutano wa Magavana wa Benki hiyo mjini Rome, Italia, baada ya mahitaji ya nchi wanachama ya kutafuta mikopo kwenye taasisi hiyo kuongezeka.(Benny Mwaipaja, WFM, Washington DC)
Ad

Unaweza kuangalia pia

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *