MILIONI 700 ZAANZA KUTOA MATOKEO CHANYA KATIKA UKARABATI WA CHUO CHA MAOFISA WA POLISI Matokeo ChanyA+ May 8, 2019 Tanzania MpyA+ Acha maoni 1,617 Imeonekana Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akipita kukagua ujenzi wa majengo mapya na ya kisasa yanayojengwa katika Chuo cha Maofisa wa Polisi kilichopo Kurasini jijini Dar es salaam, ujenzi unaotokana na fedha iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, kiasi cha shilingi milioni 700 kwa ajili ya ukarabati wa Chuo hicho cha Maofisa. Picha na Jeshi la Polisi. Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akifurahia jambo huku akiwa amembeba mtoto aliyefika katika hospitali Kuu ya Polisi iliyopo Kurasini jijini Dar es salaam leo, akiwa na mzazi wake kwa ajili ya kupata huduma za matibabu hospitalini hapo, IGP Sirro amefanya ziara ya ghafla ya ukaguzi yenye lengo la kuona namna huduma za matibabu zinavyotolewa pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo. Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (kulia) akizungumza na Maofisa wa Polisi wanaofanyakazi katika hospitali Kuu ya Polisi iliyopo Kurasini Dar es salaam leo, wakati alipofanya ziara ya ghafla ya ukaguzi yenye lengo la kuona namna huduma za matibabu zinavyotolewa pamoja na changamoto wanazokutananazo ambapo IGP Sirro amewataka viongozi hao kutoa huduma bora kwa wateja. Ad Share Facebook Twitter Stumbleupon LinkedIn Pinterest