
- Tanzania imeshika nafasi ya nne kati ya nchi tisa za Kusini na Mashariki mwa Afrika zilizofanyiwa utafiti kwa kuwa na asilimia 64 ya watu wanaoamini kuwa hali ya umiliki wa ardhi na makazi ni salama.
- Hayo yalibainika wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Msingi kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, uzinduzi ulifanyika jijini Dodoma.
- Akizungumza wakati wa kuzindua Ripoti hiyo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema kiwango hicho ni kikubwa zaidi ya wastani wa asilimia 61 kwa nchi tisa zilizofanyiwa utafiti katika Afrika ya Magharibi.
- Aidha, Utafiti wa Ripoti hiyo unaonesha Tanzania imeshika nafasi ya kumi kati ya nchi 33 zilizoshiriki katika Utafiti huo kwa kuwa na asilimia zaidi ya hamsini ya watu wanaomiliki makazi yao wenyewe.
- Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, matokeo ya utafiti huo yametokana na hatua mbalimbali ambazo serikali imeendelea kuzichukua ili kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na usalama wa umiliki wa ardhi na makazi.Na Munir Shemweta, DODOMA
Ad