SERIKALI KUFANYA UKAGUZI NA TATHMINI YA KINA YA MIRADI YOTE YA UMWAGILIAJI NCHINI – MHE MGUMBA

  • Serikali iko katika mchakato wa kufanya ukaguzi na tathmini ya kina ya miradi yote ya umwagiliaji nchini ili kufanya uhakiki wa eneo la umwagiliaji kwa lengo la kubaini ubora wa miradi, thamani ya fedha, gharama za mradi na mahitaji halisi ya sasa ya kuboresha, kuendeleza na kuongeza miradi mipya ya umwagiliaji.
  • Aidha, baada ya tathmini hiyo Serikali itaendelea kutafuta fedha ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha mabwawa na skimu za umwagiliaji nchini ikiwemo mradi wa umwagiliaji katika bonde la Mkomazi zinaendelezwa na kuwanufaisha wananchi wa Mombo na taifa kwa ujumla.
  • Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 16 Mei 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Mhe Timotheo Mnzava aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali katika utekelezaji wa mradi wa Umwagiliaji katika Bonde la mto Mkomazi.

    BK

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 16 Mei 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma.

  • Alisema kuwa katika miaka ya 1980 Serikali kupitia washirika wa maendeleo, Wakala wa Ushirikiano wa Kitalaam wa kimataifa wa Serikali ya Ujerumani (Germany Agency for Technical Cooperation Ltd) ulifanya upembuzi yakinifu (Feasibility studies) kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji katika Bonde la Mkomazi katika tarafa ya Mombo, Halmashauri ya Korogwe. Hata hivyo taarifa za upembuzi yakinifu na usanifu zilibaini kuwa ujenzi wa bwawa hilo ungesababisha kuongezeka kwa maji katika ziwa Manga na kupelekea kuzama kwa Kijiji cha Manga Mikocheni pamoja na mashamba ya wakulima.
  • Mhe Mgumba alisema kuwa kutokana na changamoto hiyo katika mwaka 2014/2015, wataalam wa ofisi ya kanda ya umwagiliaji ya Kilimanjaro walifanya mapitio ya upembuzi yakinifu na usanifu uliofanywa katika eneo hilo kwa lengo kuepusha uwezekano wa kufurika kwa Ziwa Manga, kuzama kwa Kijiji cha Manga Mikocheni na Mashamba ya wakulima kutokana na ujenzi wa bwawa. Mapitio hayo yalibaini uwezekano wa ujenzi wa bwawa na mradi wa umwagiliaji katika eneo hilo bila kuathiri wakazi wa eneo hilo. Mapitio ya usanifu huo yalibaini kuwa ujenzi wa bwawa pekee utagharimu Shilingi 1,543,736,877.
Ad

Unaweza kuangalia pia

MATUKIO YA WAZIRI MKUU BUNGENI MJINI DODOMA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *