• Jumuiya ya Watanzania UNITED KINGDOM -TZUK DIASPORA itafanya uzinduzi wa harambee na kampeni kubwa ya ununuzi wa jengo la kisasa kwa ajili ya jumuiya
  • Jengo hilo linategemewa kuwa na kila aina ya huduma za kijamii na kuitangaza Tanzania nje ya nchi
  • Akizungumzia kampeni hiyo hivi karibuni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania UK, Ndugu Abraham Sangiwa amesema uzinduzi huo utafanyika katika hoteli ya Chiltern jiji la Luton nchini Uingereza siku ya Jumamosi tarehe 22/06/2019 kuanzia saa sita mchana, na kunatarajiwa kuwepo kwa wadau mbalimbali na watanzania waishio UK na vitu mbalimbali vitanadiwa pamoja utoaji wa ahadi za kuchangia kampeni hiyo.
  • ”hili ni jambo la kihistoria na la aina yake kufanyika kwa watanzania waishio nje, hususan hapa UK, hivyo nawaomba tujitokeze kwa wingi ili kuwa sehemu ya historia ya tukio hili muhimu na kuitangaza vema nchi yetu huku ughaibuni” alisema Sangiwa