MAWAZIRI WA NISHATI WA AFRIKA MASHARIKI WAAHIRISHA MKUTANO WAO

KL 1-01
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (Meza Kuu), wakiwa katika kikao cha ndani na Wataalamu wa Nishati kutoka Tanzania, muda mfupi kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri la kisekta la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ufanyike Juni 7, 2019 jijini Arusha.
  • Mawaziri wenye dhamana na sekta ya nishati kutoka nchi sita zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wameahirisha Mkutano wao uliopangwa kufanyika Arusha, Juni 7 mwaka huu.
KL 2-01
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kushoto), akiongoza kikao cha ndani baina yake na Wataalamu wa Nishati kutoka Tanzania (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri la kisekta la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ufanyike Juni 7, 2019 jijini Arusha. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua.
  • Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa EAC anayeshughulikia Sekta ya Uzalishaji, Jean Baptiste Havugimana, ilieleza kuwa Mkutano huo utafanyika siku nyingine katika tarehe itakayobainishwa na Sekretarieti ya Jumuiya hiyo.
  • Katika Mkutano huo, Mawaziri walitarajiwa kupokea, kujadili na kuidhinisha kwa ajili ya utekelezaji, Taarifa ya wataalamu kuhusu miradi mbalimbali ya kisekta, iliyopitiwa na kuidhinishwa na Makatibu Wakuu wa Wizara za Nishati za nchi wanachama wa EAC.
KL
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (katikati) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto) pamoja na Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi, Mwanamani Kidaya, muda mfupi kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri la kisekta la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ufanyike Juni 7, 2019 jijini Arusha.
  • Hata hivyo, Mkutano huo mkubwa wa 14 wa Mawaziri wa Sekta ya Nishati wa EAC, ulifanikiwa kufanyika katika ngazi za awali ambazo huhusisha Wataalamu na kufuatiwa na Makatibu Wakuu.
  • Vikao vya Wataalamu vilifanyika katika moja ya kumbi za Ofisi za EAC jijini Arusha kuanzia Juni 3 hadi 5 na kukabidhi Taarifa yao kwa Makatibu Wakuu Juni 6, ambao nao walitarajiwa kuiwasilisha kwa Mawaziri husika Juni 7 endapo Mkutano ungefanyika.
KL
Matukio mbalimbali wakati Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakiwa katika kikao cha ndani na Wataalamu wa Nishati kutoka Tanzania, muda mfupi kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri la kisekta la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ufanyike Juni 7, 2019 jijini Arusha.
  • Katika Kikao cha Makatibu Wakuu, Tanzania iliwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua. Aidha, kwa ngazi ya Wataalamu, Tanzania iliwakilishwa na Wizara ya Nishati, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira (Zanzibar), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
  • Wengine ni Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa pamoja (PBPA), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na Kampuni ya Kuendeleza Jotoardhi Tanzania (TGDC).
  • Kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano, Mawaziri kadhaa walikuwa wameshafika eneo la tukio akiwemo mwenyeji wao, Dkt. Medard Kalemani (Tanzania), ambaye alifanya kikao cha ndani na Katibu Mkuu Mwinyimvua pamoja na wataalamu Watanzania. Na Veronica Simba – Arusha
Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI AMTEUA BALOZI WILBERT IBUGE KUWA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Balozi (Kanali) …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.