- Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.Atashasta Nditiye amazindua Rasmi Vifaa vya Kunyanyulia Makontena ya Mizigo na Vifaa vizito vya utekelezaji wa ujenzi wa Mradi mkubwa wa umeme wa Julius Nyerere Hydro Power Project (JN HPP).
- Akizungumza jana katika stesheni ya fuga, Waziri Nditiye alisema kuwa Serikali imenunua vifaa hivyo ambavyo ni Reach Stacker 2 zenye uwezo wa kunyanyua tani 45, Mobile crane yenye uwezo wa tani 15 na Forklift 2 zenye uwezo wa tani 5 na zimegharimu Tzs Bilioni 3.5
- “Vifaa hivi vimenunuliwa na Serikali ili kuiwezesha TAZARA kutekeleza majukumu iliyopewa ya upokeaji makontena ya mizigo mizito ya ujenzi wa bwawa la kufua umeme la JN HPP, katika mto Rufiji, mradi utakozalisha Megawati 2,115 na kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa viwanda”, Naibu Waziri Nditiye.
- Aidha, Waziri Nditiye alisema kuwa Serikali itaendelea kuishika mkono TAZARA ili kuhakikisha inafanya kazi ufanisi mkubwa kwenye utekelezaji wa mradi wa kufua umeme JN HPP na ndiyo maana imetoa Tsh. Bilioni 10 ili kununua Traction Motors 42 kwa ajili ya vichwa saba vya treni za masafa marefu na sogeza ambazo zitaanza kuwasili mwezi oktaoba.
- Waziri Nditiye aliongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawahakikishia wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA)kuwa itaendelea kulipa mishahara yote kwa kipindi chote cha mwaka wa fedha 2019/2020 na tayari imetanga kiasi cha shilingi bilioni 14.9 zimetengwa.
- Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) alisema kuwa ni jambo kubwa na heshima kwa Mamlaka hiyo kupewa majukumu ya kupoea mizigo ya utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa Umeme JN HPP.
- “Napenda kusema kuwa Serikali ya Tanzania, Chini ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli, ilituamini na kutupatia kiasi cha Shilingi Bilioni tano ili kukarabati stesheni ya Fuga kwa kujenga Stendi ya kupokea na kusafirisha mizigo, kununua vifaa vitakavyosaidia kunyanyua mizigo hiyo kwa ufanisi mkubwa”, Mhandisi. Bruno Chingandu.
- Mhandisi Chingandu alisema kuwa vifaa hivyo viyakuwa na uwezo mkubwa wa kutosheleza mahitaji ya kupokea mizigo ya ujenzi wa mradi mkubwa wa kihistoria wa kufua umeme wa JN HPP, kwani tani kati ya 5 mpaka 45 zitanayanyuliwa na vifaa hivyo.
- Aidha, Mhandisi Chingandu alisema kuwa Serikali imetekeleza kwa vitendo ununuzi wa Traction motor 42 kwa ajili ya treni ya masafa marefu kwa kutoa Tsh.Bilioni 10, hivyo itaiwezesha TAZARA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa na kuliwezesha Shirika hili kurejera tena katika utendaji mkubwa.
- Naye Meneja wa TAZARA Mkoa wa Tanzania, Fuad Abbdalah, alisema kwamba Serikali imewapatia Fedha za ujenzi na ununuzi wa vifaa ni heshima kubwa kwa Shirika hilo kwani limeingia kwenye historia ya mageuzi ya Serikali ya Awamu ya Tano.
- “Leo tunashuhudia kitendo kikubwa cha kuzindua hizi mashine tano za kunyanyulia mizigo mizito ya ujenzi wa Mradi wa kihistoria wa JN HPP, Mashine hizi zina uwezo mkubwa wa kunyanyua Tani 5 mpaka 45, uwezo stahiki kabisa kuhudumia mizigo yote inayohitajika kwenye mradi wa umeme mto Rufiji”; Fuad Abbdalah, Meneja TAZARA mkoa wa Tanzania
- Fuad aliongeza kuwa Serikali imeliamini Shirika hilo na Rais wa Jamhuri ya Muungano ameahidi kurudisha uafanisi wa utendaji wake na katika ziara yake ya kwenda kuzindua Mradi wa umeme JN HPP alisema atahakikisha anashirikiana na Rais wa Zambia ili kurudisha heshima ya TAZARA.
- Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi alisema Serikali imetekeza ukarabati wa stesheni ya kupokea na kushushia mizigo ya Fuga itayosaidia ujenzi wa Mradi wa Umeme wa JN HPP kufanikiwa kwa haraka Zaidi.
- “Tunatekeleza Uboreshaji huu wa Stesheni ya Fuga, tumeleta mitambo ya kisasa mikubwa kabisa ambayo imedhaminiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kuhudumia ujenzi wa bwawa la kufua umeme JN HPP, kwa hiyo mitambo hii imefika, inafanya kazi na inasambazwa na Kampuni ya kizawa”, Dkt.Abbasi.Na.Paschal Dotto-MAELEZO
Ad