UJENZI WA STENDI, SOKO NA ENEO LA KUPUMZIKIA JIJINI DODOMA KUKAMILIKA DISEMBA 30 MWAKA HUU.

  • Mkuu wa Mkoa wa Dodoma dkt Binilith Mahenge amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi ya uendelezaji miji mkakati(TSCP) inayotekelezwa jijini Dodoma ambayo ujenzi wake kwa sasa umefikia asilimia 75.
  • Akizungumza leo agosti 30 baada ya kukagua ujenzi wa miradi hiyo ambayo ni eneo la kupumzikia, soko na stendi ya kimataifa dkt Mahenge amesema anaona faraja kufanya kazi na mkandarasi mzawa aliye mzalendo kwa nchi yake.

DD 1-01

  • “Naomba nitoe pongezi kwa mkandarasi Mohammed Builders, anajenga miradi mitatu kwa wakati mmoja na yote inaenda vizuri tena kwa ubora, kwa kweli mimi nimeridhika, naona faraja kufanya kazi na mkuu wa wilaya na mkurugenzi wake wanaosimamia vizuri miradi hii, “alisema dkt Mahenge.
  • Pamoja na pongezi hizo ameshauri mambo matatu, moja ni kuheshimu maeneo ya wazi yaliyopo kwa kuyatambua, kuyaorodhesha na kuwasilisha orodha hiyo ofisini kwa katibu tawala wa mkoa wa Dodoma ili kutambua maeneo hayo kama yapo.

DD 2-01

  • “Lazima tuheshimu maeneo ya wazi, ipatikane orodha ya open space zote katika jiji hili, na kusiwe na mtu anayevamia maeneo hayo yaliyotengwa, kama kuna mtu amejenga ajiandae kuondoka,”alisema dkt Mahenge.
  • Ameutaka uongozi wa jiji kuweka utaratibu wa uendeshaji miradi hiyo ili inapokamilika taratibu nyingine pia ziwe zimekamilika.

DD 3-01

  • “Uwekezaji huu ni mkubwa ni lazima jiji muanze kuandaa namna ya kuuendesha, sisi watanzania usipoweka vizuri utaratibu soko hili na stendi utashangaa yanachafuka, ningeshauri muanze kuratibu leo,”alisisitiza dkt Mahenge.
  • Akitoa maelezo ya miradi hiyo mkurugenzi mtendaji wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi amesema miradi hiyo inatekelezwa kwa gharama ya sh bilioni 77.8.
  • “Miradi hii inaendana na hadhi ya makao makuu na ni miradi bora kabisa, Dodoma tunayoijenga sasa baada ya mwaka 1 au 2 itakuwa ni eneo ambalo mtu atataka kuja kutembea na kutalii, alisema Kunambi.

DD 4-01

  • Ametaja faida ya miradi hiyo kuwa ni kuongeza mapato, kuwasaidia wananchi kuweza kujiinua kiuchumi kutokana na biashara mbalimbali watakazozifanya ndani ya miradi hiyo.
  • “Katika miradi hii tumewajali wafanyabiashara wadogo,katika eneo la stendi machinga watakuwa na sehemu yao,kutakuwa na supermarkets, hoteli,sehemu ya kuegeshea magari, eneo la soko halikadhalika miundombinu mbalimbali itakuwepo na hivyo kuwa sehemu ya kuzalisha ajira,”aliongeza Kunambi.

DD 5-01

  • Kwa upande wake mhandisi Emmanuel Mahimbo kutoka kampuni ya Mohammed Builders amesema ujenzi wa miradi hiyo ulianza julai mwaka jana na ilikuwa ikamilike septemba 30 mwaka huu lakini kutokana na baadhi ya changamoto miradi hiyo itakamilika disemba 30 mwaka huu.

DD 7-01

  • “Awali tulipoanza kulikuwa na changamoto ya kokoto kutokana na ujenzi uliokuwa unaendelea ukiwemo mji mkuu wa serikali, na kuongezeka baadhi ya kazi ambazo awali hazikuwepo lakini mpaka disemba 30 kazi zote kwenye miradi hii mitatu itakuwa imekamilika,”alisema mhandisi Mahimbo.
  • Nae mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi amemshukuru Rais John Magufuli kwa kupeleka fedha nyingi za utekelezaji wa miradi na kuahidi kusimamia utekelezaji wa sera, mipango na mikakati.

DD 8-01

  • “Mimi kama msimamizi mkuu wa wilaya niahidi kusimamia,utekelezaji wa Ilani  uliofanyika wilayani kwetu ni wa asilimia 99.9, zawadi yetu kwa Rais ni kumuombea,  kuchapa kazi,na kuhakikisha kura zetu zisizo na idadi anazipata katika chaguzi zijazo,”alisema Katambi.

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI KUTOINGILIA TAALUMA YA UKAGUZI WA HESABU ZA FEDHA

Serikali imeeleza kuwa haina mpango wa kuingilia taaluma ya ukaguzi wa hesabu nchini kwa kuondoa …

Oni moja

  1. Very interesting details you have mentioned, thank you for putting up.Raise blog range

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *