DKT.KALEMANI ATOA MWEZI MMOJA NGUZO ZILIZOHIFADHIWA ZISAMBAZWE

  • Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani amewagiza mameneja wa Shirika la Umeme Nchini(TANESCO)wote nchini kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja wanasambaza kwa wateja  nguzo zote za akiba zilizohifadhiwa  katika vituo na maeneo mbalimbali nchini.
  • Kalemani alisema hayo, Septemba 28,2019, baada ya kuona nguzo zaidi ya Elfu mbili zikiwa zimehifadhiwa katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida, wakati wa ziara yake ya  kukagua ujenzi upanuzi wa kituo hicho kinachojengewa uwezo wa kupoza na kusambaza umeme wa  Kilovolti(kV) 400.
N 1-01
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani( katikati) akikagua nguzo zilizo hifadhiwa katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida
  • Dkt.Kalemani, alisema kuwa hapendezwi kuona wateja wanalalamikia suala la ukosefu wa nguzo na kushidwa kuunganishiwa umeme katika maeneo mbalimbali wakati kuna nguzo zimerundwika mahali kwa ajili ya matumizi ya akiba.
  • “Wananchi wanahitaji nguzo kila siku,mnawaambia hakuna nguzo, ajabu nguzo kama hizi zimehifadhiwa sehemu mbalimbali mnadai ni za matumizi ya akiba,sasa akiba ya nini wakati wananchi bado wanauhitaji , pia maeneo  mengi nguzo zimeharibika zinataka kubasilishwa, nawapa Mwezi mmoja zisionekane hapa na maeneo mengine yote!”, Alisema Dkt.Kalemani.
N 3-01
Vibarua wakiendelea na kazi ya ujenzi wa upanuzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida, wakati Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani, alipofanya ziara ya kukagua shughuli za ujenzi katika kituo hicho.
  • Katika hatua nyingine, alimtaka mkandarasi wa Kampuni ya KC International LTD inayotekeleza ujenzi wa upanuzi wa Kituo cha Kupoza na kusambaza umeme cha Singida kuongeza nguvu kazi ili kuharakisha ujenzi wa kituo hicho ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Januari 2020.
  • Kazi ya ujenzi katika hatua ya awali katika kituo hicho imekamilika na kufikia 95% ambapo pia  tayari wamekamilisha baadhi ya maeneo zitakaposimikwa transofoma kubwa nne ambapo mbili kati ya hizo zitakuwa na uwezo wa 125 MVA kwa kila moja na mbili nyingine zitakuwa na uwezi wa 250 MVA kila moja, pia kazi ya kukamilisha ujenzi wa jengo la kuendeshea mitambo inaendelea
N 4-01
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani, akitoa maelezo kwa Mkandarasi na wasimamizi katika Ujenzi wa upanuzi wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida, baada ya kukagua shughuli za ujenzi zinazoendelea katika kituo hicho.
  • Mradi huo ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa Megawat(MW) 432 ambapo kwa sasa mahitaji ya umeme kwa Mkoa wa Singida ni MW 15 tu, hivyo kituo hicho kitaimarisha upatikanaji wa Umeme wakutosha na wauhakika katika Mkoa huo na mikoa iliyo karibu.
  • Kituo cha Kupoza na kusambaza umeme cha Singida ndiyo kitakuwa kituo kikubwa na pia  njia panda kubwa ya kusambaza umeme kwenda katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa kupitia Mkoa wa Shinyanga, Kanda ya Kaskazini kupitia Babati Mkoani Manyara, hadi Namanga Mkoani Arusha na baadaye Nchini Kenya.
  • Gharama za upanuzi wa kituo hicho ni Dola za Kimarekani milioni 60 sawa na Bilioni 130 za Kitanzania, fedha hizo ni mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB), Shirika la Maendeleo la Japan(JICA) pamoja na Fedha za ndani.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI KALEMANI AFUNGUA KIWANDA CHA NGUZO ZA UMEME – KIGOMA

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amefungua kiwanda cha Nguzo cha Qwihaya, kilichopo katika Mtaa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *