RAIS MAGUFULI: SISI TUNAUWEZO, FURSA NA MAZINGIRA YA KUINGIA KWENYE USHIRIKIANO MADHUBUTI WA KIUCHUMI

  • Mustakabali wa Taifa letu hauwezi kuwa na maana sana, endapo taifa letu litaendelea kuwa tegemezi kiuchumi.
  • Pamoja na uhusiano mzuri na mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye ushirikiano kati ya nchi za Afrika na Nordic, bado tuna fursa ya kuukuza uhusiano wetu na kuupa msukumo mpya ili kuleta manufaa makubwa zaidi kwa pande zetu mbili. Na suala hili ni muhimu kwa sababu, kwa muda mrefu, ushirikiano wetu umejikita zaidi kwenye kutoa na kupokea misaada, yaani donor-recipent relationship.
  • Ushirikiano wa aina hii siyo endelevu na wala hauhitajiki katika mazingira ya sasa. Viongozi wengi wa Afrika tumetambua kuwa mustakabali wa Bara letu uko mikononi mwetu na kwamba uhuru wa kisiasa hauwezi kuwa na maana sana, endapo mataifa yetu yataendelea kuwa tegemezi kiuchumi. Hatuwezi kuwa na uhuru wa kujiamlia mambo yetu wenyewe endapo mataifa yetu yataendelea kuwa ombaomba.
  • Kutafuta ukombozi wa kiuchumi ndilo jukumu tuliloachiwa sisi viongozi wa sasa wa Africa. Hata Hayati Mwalimu Julius Nyerere alisema, katika moja ya hotuba zake kwamba “The first generation of leaders led Africa to political freedom. But we, the current generation of leaders, must pick up the flickering torch and lead Africa towards economic liberation”.  
  • Hivyo basi, ni lazima tubadilishe mwelekeo na kuingia kwenye uhusiano wa kisasa baina ya mataifa ambao unajikita kwenye ushirikiano wa kiuchumi (economic partnership) kupitia biashara na uwekezaji. Diplomasia ya uchumi ndiyo iwe msingi wa uhusiano na ushirikiano baina ya mataifa yetu.
  • Kwa bahati nzuri, uwezo, fursa na mazingira ya kuingia kwenye ushirikiano madhubuti wa kiuchumi yapo. Kwa mfano, nchi za Nordic, ambazo zipo tano: Denmark, Finland, Iceland, Norway na Sweeden; licha ya kuwa na eneo dogo (kilomita za mraba milioni 3.5) na idadi ya watu wapatao milioni 27 tu; zina uchumi mkubwa. Pato lao kwa mwaka jana (2018) lilikuwa na thamani ya Dola za Marekani trilioni 1.7.
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *