NAIBU WAZIRI MGALU: TANESCO NA REA, MSIACHE KIJIJI HATUTARUDI NYUMA

  • Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijiji (REA) kuhakikisha hawaruki kijiji katika REA Awamu ya Tatu mzunguko wa Pili unaoanza mapema mwezi Januari 2020 kwa kuwa awamu hii ni ya mwisho kuunganisha Vijiji.
2-01
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizungumza na wakazi wa Kijijizi cha Migude, Kata ya Kiromo, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, alipofika kuwasha umeme katika kijiji hicho.
  • Mgalu alisema hayo, Desemba 8, 2019 wakati akiwasha umeme katika Kijiji cha Migude, Kata ya Kiromo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
  • Mgalu alifafanua kuwa katika utekelezaji wa REA Awamu ya Tatu mzunguko wa Pili ni wa mwisho katika kusambaza umeme vijijini, miradi itakayofuata ni kusambaza umeme katika Vitongoji, hivyo REA na TANESCO wahakikishe wanashirikisha Serikali za Mitaa ili kuorodhesha vijiji vyote kwa umakini na usahihi ili viweze kupatiwa umeme ifikapo  Mwezi, June 2021.
4-01
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( pili kushoto) akikata utepe kuashiria kuwasha umeme katika Kijiji cha Migude, Kata ya Kiromo, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, alipofika kuwasha umeme katika kijiji hicho.
  • Alieleza kuwa huenda Tanzania inaongoza  kwa kuwa ya nchi ya kwanza kwa  nchi za Afrika Mashariki katika kusambaza umeme vijijini, ambapo  mpaka sasa ina vijiji 8115, vilivyounganishwa na umeme kati ya vijiji  12,000,  vijiji 4000 vilivyosalia  kazi ya kusambaza umeme na kuwaungaishia wateja inaendelea ili kufikia  Mwezi Juni 2020 vijiji 10336 viwe  vimeunganishiwa umeme na kubakiwa na  vijiji  1,200 ambavyo hivi vitaendelea kuunganishiwa  umeme  hadi kufia mwezi June 2021, vijiji vyote nchini vitakuwa vimeunganishwa na umeme.
  • “TANESCO na REA, hakikisheni hamuachi kijiji, hii ni awamu ya mwisho kwa mradi wa REA mzunguko wa tatu, “Hii ndiyo Baba lao”, hatutarudi nyuma tena kuunganisha vijijini, miradi itakayokuja sasa itakuwa ni maalum kwa ajili ya vitongoji, hivyo basi mshirikishe serikali za mitaa kuhakikisha hakuna kinachoachwa nyuma na bei ya kuunganishiwa umeme ni shilingi 27,000, na ni marufuku kuwauzia wateja Nguzo wala LUKU”  alisisitiza Mgalu.
5-01
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,(kushoto) akimtwika ndoo ya maji mmoja wa akina Mama wa Kijiji cha Migude, Kata ya Kiromo, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, katoka katika kisima cha maji kinachotumia umeme wa REA baada ya Naibu Waziri kuwasha umeme katika kijiji hicho.
  • Aidha aliipongeza Bodi ya Wakurugenzi ya REA, kwa kukubali na kuridhia maombi ya nyongeza ya Kaya  5000, ambazo zilizomba kuunganishiwa umeme na zoezi hilo likafanyika kwa Mkoa wa pwani,hivyo alitaka utaratibu huo uendelee kwa maeneo mengine nchini  kwa kuwa miradi hiyo imetumia gharama kubwa katika kuitekeleza na lengo ni kuwafikia wananchi wote.
  • Sambasamba na hilo aliitaka TANESCO kuangalia namna bora nzuri ya kuwawezesha wateja kulipia gharama za kuunganisha umeme katika majumba yao, ikiwezekana kuwakopesha na baadaye walipie kupitia LUKU au Ankara zao au kuwawekea utaratibu wa kulipia kidogo kidogo ili kila mmoja aweze kuunganishwa na umeme.
7-01
Mbunge wa Bagamoyo. Dkt. Shukuru Kawambwa akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Migude, Kata ya Kiromo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
  • Aliwaeleza kuwa TANESCO wasikatae fedha pale mteja anapotaka kulipa kwa awamu, isipokuwa waweke utaratibu mzuri wa walipo hayo kwa lengo la kumsadia mteja yule ambaye hawezi kuzilipa zote kwa mara moja ili aunganishiwe umeme.
  • Alirudia kusema utaratibu wa bei ya shilingi elfu 27,000 uliotolewa na Rais kwa miradi ya TANESCO inalenga wateja walio vijijini ambapo kuna miradi ya REA,lakini agizo hilo haliwahusu wateja waliopo kwenye Manispaa na Majiji katika miradi ya TANESCO inayoendela kutekelezwa  kwa sababu TANESCO inatakiwa ijiendesha kutokana na mapato yake.
6-01
Moja ya kisima cha maji kilichounganishwa na umeme wa mradi wa REA katika Kijiji cha Migude, Kata ya Kiromo, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu aliwasha umeme katika kijiji hicho.
  • Hata hivyo alisema kuwa  kwa sasa serikali inapokea maoni yanayotaka gharama ya shilingi 27,000 iwe nchi nzima, maoni hayo yatafanyiwa utafiti kwa kina na kuona namna bora ya kupunguza bei ya kuwaunganishia umeme wateja  waliopo katika  Manispaa na Miji ili kila mmoja aweze kupata huduma hiyo kwa gharama anayoweza kuimudu.
3-01
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( pili kushoto) akitoa zawadi ya mifuko ya saruji kwa viongozi wa serikali za mitaa kusaidia ujenzi wa shule ya msingi katika kijiji hicho na sehemu ya kusherehekea miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika na miaka 57 ya Jamhuri.
  •  Katika hatua nyingine, Mgalu alitumia fursa hiyo kugawa mifuko 50 ya saruji isaidie ujenzi wa shule za msingi katika kijiji hicho ikiwa kusherehekea miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika na miaka 57 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Mifuko hiyo ya saruji aliikabidhi kwa Viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Ki
  • jiji cha Migude Kata ya Kiromo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na baadaye kutembelea shule zenye uhitaji mkubwa  vifaa na miundombinu. Na Zuena Msuya ,Pwani
Ad

Unaweza kuangalia pia

TPDC YAOKOA TRILIONI 12.7 KUAGIZA MAFUTA NJE YA NCHI

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *