Maktaba ya Mwezi: December 2019

MKUU WA MKOA WA RUKWA JOACHIM WANGABO AWATOA HOFU MAWAKALA WA MBOLEA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewatoa hofu mawakala wa mbolea mkoani Rukwa kutokana na kupata changamoto ya kulipishwa kibali cha kuingiza malori katika mji w Sumbawanga huku akiwaelewesha wakulima wa mkoa huo kuwa rangi ya mbolea isiwarudishe nyuma wao kutumia mbolea bali waangalie kilichomo ndani ya mbolea …

Soma zaidi »

WAZIRI UMMY AZINDUA BODI YA TAASISI YA MAENDELEO YA JAMII TENGERU

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameizindua Bodi ya pili ya uendeshaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru na kuitaka kuleta chachu ya mabadiliko katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini. Waziri Ummy ameyasema hayo leo Mkoani Arusha wakati akizungumza na wajumbe wa …

Soma zaidi »

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI INASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA VIWANDA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inashiriki katika Maonesho ya Nne ya Viwanda yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE). Kupitia Maonesho hayo, Wananchi wanaelimishwa kuhusu majukumu ya Wizara na utekele zaji wake na namna wizara na balozi za Tanzania zinavyofanya kazi ya kuvutia …

Soma zaidi »

AGIZO LA WAZIRI KALEMANI KUPELEKA UMEME KABUKOME LAAMSHA NDEREMO

Wananchi wa kijiji cha Kabukome, Kata ya Nyalubungo, wilayani Biharamulo, Mkoa wa Kagera, wameruka kwa nderemo na vifijo, wakifurahia maagizo aliyoyatoa Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani Desemba 5, 2019, kuwa kijiji hicho kiwe kimewashiwa umeme ifikapo Januari 30 mwakani. Waziri alitoa maagizo hayo mbele ya umati wa wananchi wa …

Soma zaidi »

MAZINGIRA SI KIKWAZO KWA WAWEKEZAJI – WAZIRI SIMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima amesema Serikali imefanya mapitio ya Kanuni ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira ili kurahisha uwekezaji nchi. Akizungumza na Wafanyabiashara na Wawekezaji katika Mkutano  wa Mashauriano baina yao na Serikali katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani  Morogoro, Naibu Waziri …

Soma zaidi »

WAZIRI KALEMANI AKAGUA UJENZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME BULYANHULU NA KUTOA MAELEKEZO

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, Desemba 4, 2019 amekagua maendeleo ya ujenzi unaolenga kupanua kituo cha kupoza umeme Bulyanhulu, wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga na kutoa maelekezo kadhaa kwa uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na mkandarasi husika. Akiwa amefuatana na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, …

Soma zaidi »

KUNA VISHAWISHI VINGI KWA WATUMISHI MADINI – WAZIRI BITEKO

Waziri wa Madini Doto Biteko amesema kuna vishawishi na majaribu mengi kwa watumishi wa wizara ya Madini na Taasisi zote za chini ya wizara ya madini kutokana na wadau wake wengi ni wenye fedha nyingi hivyo ni rahisi kuwashawishi kwa rushwa na kupelekea mtumishi kufanya maamuzi yasiyo na maadili akisema …

Soma zaidi »

NAUMIA SANA KUONA BIDHAA AU KITU CHOCHOTE KINACHOHUSIANA NA SEKTA YA MADINI KIKIINGIZWA KUTOKA NJE – WAZIRI BITEKO

Upungufu wa madini ya Chumvi kwenye viwanda vya chumvi hapa nchini unamsikitisha waziri wa madini Doto Biteko kutokana na uwepo wa mahitaji (soko) makubwa ya wanunuzi wa madini hayo huku madini hayo yakiwa hayapatikani kwa wingi kutosheleza mahitaji kutokana na uzalishaji mdogo kutoka kwa wachimbaji wa madini hayo huku wanunuzi …

Soma zaidi »