KUNA VISHAWISHI VINGI KWA WATUMISHI MADINI – WAZIRI BITEKO

 • Waziri wa Madini Doto Biteko amesema kuna vishawishi na majaribu mengi kwa watumishi wa wizara ya Madini na Taasisi zote za chini ya wizara ya madini kutokana na wadau wake wengi ni wenye fedha nyingi hivyo ni rahisi kuwashawishi kwa rushwa na kupelekea mtumishi kufanya maamuzi yasiyo na maadili akisema pia wapo watu wanaowachonganisha watumishi wake na viongozi wake kwa kumpelekea taarifa za uongo na majungu.
 • Biteko, ameyasema hayo leo tarehe 04/12/2019 kwenye ofisi za Tume ya Madini jijini Dodoma wakati akiongea na wafanyakazi wapya 160 wa Tume ya Madini walioajiriwa hivi karibuni huku akiwahasa kuzingatia maadili ya kazi na kuepuka rushwa.
 • “Wengiwenu ni vijana, mna hari ya kufanya kazi na mna ndoto zenu. Nendeni mkafanye kazi kwa bidii kwa kuzingatia maadili ya kazi na kujituma. Rushwa ni hatari sana, wapo watakao wajaribu kwa majiribu ya kila aina, naombeni nendeni mkayaepuke hayo majaribu” alisema Biteko.
1-01
Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza na watumisha wapya 160 wa Tume ya Madini kweenye ofisi za Tume ya Madini Jijini Dodoma
 • Biteko ameongeza kuwa anaishukuru sana Tume ya Madini kwa kazi kubwa wanayoifanya..“Nakushukuru sana Prof. Manya (Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini) unafanya kazi nzuri sanaa pamoja na mwenyekiti wenu Prof. Kikula ambae hapa hayupo hakika mnanisaidia sana. Hata muda wenu ukiisha nitamuomba Mhe. Rais awabikize kwa sababu bado mnahitajika sana katika wizara hii.
 • Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila amewaambia watumishi hao wapya kuwa wanawajibu mkubwa wa kuongeza tija ya Tume ya Madini na wizara kwa ujumla hivyo kila mmoja akajitume kwa taaluma aliyoajiriwa nayo.
 • “Sina shaka juu yenu, ni vijana, mnna nguvu, mna hari ni imani yangu kuwa mtakuwa chachu katika utendaji nzuri wa kazi za wizara kwa ujumla. Nendeni mkawasikilize wasimamizi wenu, msisikilize watu watakao wapotosha, kafanyeni mnachopangiwa kufanya” alisema Prof. Msanjila.
2-01
Viongozi wa Wizara ya Madini na Tume ya Madini wakisubiri muda mfupi kabla ya kuzindua magari yaliyotolewa na serikali kwa Tume ya Madini.
 • Wakati huo huo Waziri wa Madini na Katibu Mkuu wamemshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwapatia vitendea kazi mbalimbali yakiwemo Magari, Computer na vifaa vingine vya kuthaminishia madini, na kuongeza kuwa kupewa kwa vitendea kazi hivyo ni deni na kwamba wanatamani kadirio walilopewa la kukusanya bilioni 475 kwa mwaka 2019/20 wavuke lengo hilo ili kutoa shukran kwa Rais kwa vitendo.
 • Pasipotarajiwa huku akiongea na watumishi hao, Waziri Biteko aligeuka ghafla na kuongea kwa masikitiko mazungumzo yaliyopelkea kutoa onyo kwa watumishi wanaokwamisha juhudi za Tume ya Madini na wizara kwa ujumla. Ameongeza kuwa ana taarifa ya baadhi ya watumishi kuwa na mgomo wa chinichini hasa wa idara ya Leseni.
 • “Msinifanye nifike huko mnako taka nifike, lakini kiukweli furaha yangu ya leo imeharibiwa na taarifa hii. Kuna mgomo wa chini chini ambao umesababisha mapato ya mwezi uliopita kushuka kwa sababu ya baadhi ya watu kutotimiza majukumu yao kwa makusudi”
4-01
Watumishi wapya 160 wa Tume ya Madini wakimsikiliza waziri wa Madini Doto Biteko hayupo pichani wakati wa kikao nae.
 • “Prof. Manya, nakuagiza, wale watumishi 4 uliowaleta kutoka mikoani kuja hapa makao makuu kufanya kazi wakati wenyewe wapo hapa hapa makao makuu, kuanzia leo, watumishi wale 4 wabaki hapa moja kwa moja na wale waliogoma wapeleke mikoani na juma tatu nataka ripoti ya utekelezaji wa agizo hili” alisema Biteko akionyesha kutoridhishwa na kitendo hicho.
 • Biteko aliongeza kuwa mgomo huo umeathiri Leseni 3410 zimekwama kutokutolewa kwa sababu ya mtu eti, mpaka aonwe kwa namna fulani. Ameongeza kuwa watu wenye leseni hizo wanalia na kulalamika na kuisababishia mapato Tume ya Madini.
 • Katika mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa waandamiza wa wizara ya madini na Tume ya Madini. Na Issa Mtuwa – Dodoma
Ad

Unaweza kuangalia pia

SOKO LA MDINI ULANGA LA KUSANYA MILIONI 396 NDANI YA MIEZI 5

Waziri wa Madini Doto Biteko amesema tangu kuanzishwa kwa soko la madini Ulanga wamenunua madini …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *