- Wadau wote kupitia vyama vyao waitwa kuleta mapendekezo ili kuboresha sekta zao ikiwa Serikali ipo kwenye maandalizi ya bajeti ukizingatia pia Wizara ya Viwanda na Biashara inatekeleza mpango kazi wa Blue Print ili kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.
- Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Mhe Stella Manyanya alipokuwa akifunga mkutano wa wadau wa umoja wa wazalishaji na wasindikaji wa muhogo Tanzania (TACAPPA) katika mkutano wa wadau wa muhogo ulioandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) jijini Dar es Salaam.
- “Tozo zipatazo 114 ziliondolewa kwa mwaka 2017/2019, tozo 5 zimeondolewa mwaka 2018/2019 na tozo 54 zimeondolewa kwa mwaka 2019/2020 ikiwemo kuhamisha jukumu la usimamizi wa ubora wa chakula kutoka TFDA kwenda TBS” amesema Mhe Manyanya
- Amezielekeza taasisi zake kushirikiana ili kutoa mafunzo ya usindikaji kwa wazalishaji, alama ya ubora wa bidhaa, kubuni teknolojia rahisi na kuwatafutia masoko ikiwa ni wakati muafaka wa kuwekeza katika mnyororo wa thamani wa zao la muhogo
- Nae, Mwenyekiti wa Umoja huo Bi Mwantumu Mahiza ameeleza kuwa umoja upo kwenye hatua ya kukamilisha andiko kwenda Serikali za mitaa ili shule za sekondari za bweni zilime mihogo kwaajili ya mahitaji ya chakula, kuwajenga elimu na maarifa ya kilimo bora cha muhogo kwa vijana ili waweze kujitegemea.
- TanTrade imesmamia uanzishwaji na usajili wa Chama cha Wazalishaji na Wasindikaji wa Muhogo Tanzania, lengo ni kuwa na sauti ya pamoja katika kuendeleza zao hilo.
Ad