Mbunge wa jimbo la Mtama Mkoani Lindi, Nape Nnauye amesema kuwa msimu huu kwenye zao la korosho umeenda vizuri baada ya Serikali kuviachia vyama vya Ushirika kususimamia.
Amesema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Kilimo, amesema kuwa namna bora ya kuimarisha Vyama vya Ushirika ni kuvisimamia vifanye majukumu yake na kuongeza kuwa hata suala la kuviachia vyama hivyo kununua pembejeo ni jambo nzuri kwani ni eneo lao.
“kwasababu ndio eneo lao, wao wanajua mahitaji, wakulima ni wa kwao, uchungu ni wa kwao ninyi simamieni tu mambo yaende sawa lakini wafanye wao” Amesema Nape
Aidha, Nape ameiomba Serikali kuviachia Vyama vya Ushirika kwenye suala la kununua magunia kwani vyama hivyo vinauwezo wa kuingia mikataba na mabenki na Serikali isimamie suala hilo kwa kuwaelekeza Vyama hivyo magunia yanakopatikana
Akizungumzia suala la maonesho ya wakulima 88 Nape amesema kuwa ni wakati sasa wa Serikali kuanzisha mashamba darasa kwenye kata kama ambavyo Ilani ya inavyosema ili kuweza kumfikia mkulima aliko kwani wakulima hawawezi kufika katika maonesho na ya nane nane badala yake wafatwe kwenye kata zao.