TANESCO KUTUMIA BIL.1.2 KUBORESHA UMEME KIWANDA CHA SUKARI MTIBWA

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa serikali imetenga shilingi za kitanzania Bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme utakaokuwa ukitumiwa na kiwanda cha sukari peke yake, katika kuendesha shughuli za uzalishaji. 

Amesema hayao alipotembelea kiwanda cha Sukari Mtibwa, ambapo amesema kuwa njia hiyo ya umeme inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi sita kuanzia mwezi Mei mwaka huu, ambayo itasaidia kiwanda hicho kupata umeme mwingi na kutosha kukidhi mahitaji ya kiwanda na ziada kwa zaidi ya miaka mitano ijayo.

Ad

“Kilichonileta hapa ni kuwajengea njia ya umeme wenu peke yenu, tumeshakaa na wataalam ili kumaliza tatizo hili, umeme hapa unatoka Msamvu takribani Kilomita 100 na unatumiwa na watu wengi, fedha tayari imekwisha tengwa na ujenzi utanza keshokutwa (Mei 13,2020) ili kukidhi mahitaji yenu ya kutaka umeme takribani Megawati 27 kwa miaka 5 ijayo, sasa lazima tuwape zaidi bila shaka mtatanua kiwanda hichi hapo baadaye,” alisema Dkt. Kalemani.

Kwa sasa kiwanda cha sukari Mtibwa kinapata Megawati 5 hadi 8 ambao pia wakati mwingine unakuwa na nguvu ndogo kutokana na kusafiri umbali mrefu pia umekuwa ukikatika kusababisha uharibifu wa vifaa na kutokidhi mahitaji ya uzalishaji.

Kiwanda hicho kilijengwa mwaka 1954 na kuanza uzalishaji mwaka 1963 hadi sasa, kinauwezo wa kuzalisha tani 200 hadi 35 za sukari kwa siku, matarajio ni kuzalisha tani 1000 kwa siku kwa kuwa wanafanya ukarabati na kuboresha miundombinu kiwanda hicho ikiwemo umeme.


Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Umeme wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa, wakati Waziri alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho kufahamu hali ya upatikanaji wa umeme, Mei 11, 2020 mkoani Morogoro. Na Zuena Msuya
Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *