NAIBU WAZIRI MABULA ATAKA WADAIWA SUGU KODI YA ARDHI KUBANWA

Na Munir Shemweta, WANMM IRINGA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinapeleka hati za madai ya kodi ya pango la ardhi kwa wadaiwa sugu wa kodi hiyo kuanzia jumatatu tarehe 18 Mei 2020 na watakaokaidi kulipa kwa hiari wafikishwe kwenye Mabaraza ya Ardhi ya Nyumba ya Wilaya.

Ad

Dkt Mabula alitoa maagizo hayo tarehe 16 Mei 2020 akiwa katika ziara yake mkoani Iringa kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi sambamba na kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika baadhi ya Taasisi zilizopo katika halmashauri za Manispaa na wilaya ya Iringa.

Katika ziara yake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwafikia wadaiwa sugu wakubwa wa mkoa wa Iringa  ambao ni Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka mkoa wa Iringa (IRUWASA) , Shirika la Umeme mkoa wa Iringa, Benki ya CRDB, Hoteli ya Peacoc  na kituo cha Radio cha EBONY ambao kwa pamoja wanadaiwa zaidi ya milioni 128.

Naibu Waziri wa Adhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka mkoa wa Iringa (IRUWASA) Gilbert Kayange taarifa inayoonesha kiasi cha kodi ya pango la ardhi inachodaiwa Mamlaka hiyo tarehe 16 Mei 2020 wakati wa zoezi lake la kuwafikia wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi katika mkoa wa Iringa

Dkt Mabula alizitaka idara za ardhi katika halmashauri zote nchini kupitia kumbukumbu za wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi vizuri na kuwaandikia Hati za Madai zitakazowataka wadaiwa kulipa kwa hiari madeni yao na watakaokaidi wafikishwe katika Mabaraza ya Ardhi ya Nyumba ya Wilaya.

‘’ Wdaiwa wote sugu wa kodi ya pango la ardhi baada ya hati ya madai kupelekwa wawe wamelipa kodi hiyo kwa hiari ndani ya siku kumi na nne na wakishindwa wafikishwe kwenye mabaraza ya ardhi ya nyumba ya wilaya, tunataka Ikifika juni 30, 2020 Wizara iwe imekamilisha kukusanya Bilioni 180 kama ilivyojiwekea katika malengo yake’’ alisema Dkt Mabula

Akiwa ofisi za Shirika la Umene mkoa wa Iringa, Naibu Waziri wa Ardhi alimueleza Meneja wa mkoa wa Shirika hilo Richard Swai kuwa, shirika lake linadaiwa milioni 384 kama kodi ya pango la ardhi kwa kushindwa kulipa kodi hiyo katika kipindi cha miaka mitatu katika eneo inalomiliki la Mtera na kutaka kupewa ahadi ya maandishi itakavyofanikisha kulipa deni hilo.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimsikiliza Mtaalamu Mshauri wa Mradi wa Kurasimisha Ardhi Vijijini unaotekelezwa na Shirika la Feed the Future Bw. Malaki Msigwa (Kulia) alipotembelea Masijala ya Ardhi ya Halmashauri ya wilaya ya Iringa wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi tarehe 16 Mei 2020.

Meneja wa TANESCO Iringa Swai alieleza kuwa, eneo linalodaiwa liko chini ya idara ya Uzalishaji Makao Makuu na malipo yake hufanywa huko ambapo alimuahidi Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kulifanyia kazi suala hilo.

Kwenye ofisi za Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Iringa (IRWASA) Dkt Mabula baada ya kumueleza Mkurugenzi wake Gilbert Kayange kuhusiana na deni la Mamlaka hiyo katika maeneo ya Gangilonga na Itamba linalofikia milioni 104.1, Mkurugenzi huyo alisema, Mamlaka yake  imekuwa ikilipa kodi hiyo ingawa kuna tofauti ya kiwango cha deni walichopelekewa na kumbukumbu walizo kuwa nazo jambo alilolieleza kuwa limeifanya Mamlaka yake kutaka kukaa pamoja na halmashauri husika ili  kufanya uhakiki.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *