KITUO KIKUU CHA MABASI CHA DODOMA KUZINDULIWA HIVI KARIBUNI – MKURUGENZI WA JIJI LA DODOMA

Sehemu ya ndani ya Kituo Kikuu cha Mabasi cha Dodoma inavyoonekana baada ya kukamilika

Charles James, Michuzi TV

Jiji la Dodoma limesema ifikapo Juni 30 mwaka huu ndio itakua mwisho kwa Mabasi makubwa ya abiria kupaki nje ya Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi katika mkutano wake na wandishi wa habari wakati alipotembelea Ujenzi wa Kituo hicho kinachojengwa katika eneo la Nzuguni.

Eneo la VIP katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Dodoma ambalo lina Mgahawa na Bar kama ambavyo linaonekana

Kunambi amesema ujenzi wa Kituo hiko ambacho kitakua kikubwa kuliko vyote kwa ukanda wa Afrika Mashariki tayari umekamilika na muda wowote kuanzia sasa wananchi watatangaziwa tarehe ya kuanza kutumika.

Amewataka wamiliki wa Mabasi wote kuhakikisha mabasi yao yanapaki katika Kituo hiko na ambaye atalaza nje ya hapo ni lazima awe na eneo lake maalum (yard) ambayo Jiji la Dodoma itakua imeipitisha.

” Kukamilika kwa ujenzi huu kunaenda kuipa hadhi Jiji la Dodoma ambalo ndio Makao Makuu ya Nchi na Serikali, hivyo hatuna muda kumshukuru Rais Magufuli ambaye yeye ndiye hasa amechangia kupatikana kwa kituo hiki.

Ad
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi akizungumza na wandishi wa habari leo katika eneo la Kituo Kikuu cha Mabasi ambacho kinatarajiwa kuanza kazi hivi karibuni. (picha na Charles James, Michuzi TV)

Uwepo wa Kituo hiki kutainufaisha Halmashauri yetu kimapato na pia kuinua maisha ya wananchi wetu ambao wengi wao wameomba nafasi ya kuwekeza biashara zao ndani ya kituo hiki na tayari wenye sifa wameshapatikana na kuanzia kesho tutaweka majina yao hadharani kwenye ubao wa Jiji na kwenye mitandao,” Amesema Kunambi.

Amesema Kituo hiko kina hadhi ya kimataifa ndio maana kina eneo maalum la VIP ambalo wasafiri wanaweza kusubiri Mabasi yao wakiwa hapo wakiangalia televisheni, kula na kunywa kupitia migahawa ya kisasa iliyopo lakini pia kupumzika.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA SULUHU AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAZIRI WA NCHI, WIZARA YA MAMBO YA NJE YA SHIRIKISHO LA JAMHURI YA UJERUMANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akizungumza na kuagana na …

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.