SERIKALI YAWATAKA MAAFISA MADINI KUTHIBITISHA USHURU MIGODINI

Waziri wa Madini Doto Biteko akikagua shughuli za uchimbaji madini katika eneo la Lusu, wilayani Nzenga Mkoa wa Tabora.

Serikali imesema Ushuru wowote unaotolewa kwenye Maeneo ya Migodi Nchini ni lazima uthibitishwe na Maafisa Madini walioko kwenye maeneo husika.

Tamko hilo lilitolewa Mei 24, 2020  na Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akizungumza na Wachimbaji  Wadogo wa Madini ya Dhahabu eneo la Lusu Wilayani Nzega  Mkoa wa Tabora alipotembelea eneo hilo kuangalia shughuli za uchimbaji madini.

Ad

Aidha, tamko hilo linafuatia kuwepo kwa malalamiko toka kwa wachimbaji wanaofanyakazi kwenye Leseni za baadhi ya Wachimbaji ambao walimlalamikia Waziri Biteko kutozwa kodi na wenye leseni hizo na hivyo kuomba ufafanuzi juu ya suala hilo.

Waziri Biteko alisisitiza kwa kuwataka Maafisa hao kuhakikisha  Ushuru unaotolewa ni ule tu uliopo Kisheria na kuhakikisha wanasimamia jambo hilo.

Baadhi ya Wachimbaji wakimwangalia Waziri Biteko (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika migodi ya Lusu Wilayani Nzega

Na Asteria Muhozya, Nzega

Akifafanua kuhusu suala la mrabaha wa mawe  unaotozwa na Serikali alieleza kuwa,  wachimbaji wasio rasmi  wanalazimika kulipia mrabaha wa mawe isipokuwa wenye Leseni wanatakiwa kulipia mrabaha wa dhahabu baada ya kukamilisha hatua zote.

” Wale msio rasmi mjue mkigawana mawe na  Serikali  itakuwepo mnagawana nayo isipokuwa mwenye Leseni  yeye tutamwomba mrabaha wetu mwishoni. Ukitaka kulipa mrabaha mara moja chimba kwenye Leseni, mkichimba bila utaratibu tutagawana kwenye mawe na kwingine,” alisisitiza Waziri Biteko.

Pia, aliendelea kuwasisitiza wachimbaji nchini kuyatumia Masoko ya Madini yaliyoanzishwa katika maeneo mbalimbali kufanya biashara ya madini.

Akijibu ombi la wachimbaji hao kupelekewa Wataalam wa masuala ya Utafiti ili kuwawezesha kujua  mwelekeo wa miamba na hivyo kuchimba kwa tija, alisema Wizara itaangalia namna ya kufikisha Mtambo wa  Kuchoronga katika eneo hilo baada ya Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) kukamilisha kazi za kandarasi za uchorongaji zinazoendelea  katika maeneo mengine.

Katika hatua nyingine, alipongeza wachimbaji kwa kulipa mrabaha wa Serikali na hivyo kuwezesha makusanyo ya  shilingi Bilioni 2.7 hadi  kufikia Aprili 30, sawa na asilimia 122 na hivyo  kuvuka lengo la makusanyo ya shilingi bilioni 2.2 zilizopangwa kukusanywa Mwaka wa fedha 2019/2020.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *