RC KAGERA AKABIDHI BOTI KWA WATENDAJI KATA, ATOA MAAGIZO KUHUSU MATUMIZI

Na Allawi Kaboyo,Muleba

Kufatia kuwepo kwa vitendo vya uvuvi Haramu katika ziwa Victoria,Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amekabidhi boti tatu mpya kwa watendaji wa Kata za Bumbire na Ikuza na boti moja kubwa kwa sekta ya uvuvi kwa lengo la kudhibiti uvuvi haramu wilayani Muleba.

Zoezi hilo lilifanyika katika kijiji cha Katembe Kata Nyakabango wilayani Muleba ambapo mkuu huyo aliipongeza halmashaurihiyo kwa jitihada kubwa inazozifanya katika kuhakikisha serikali inaendelea kupata mapato hasa kupitia uvuvi na kuzitaka halmashauri nyingine kuiga mfano huo.

“Naipongeza sana Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kwa utekelezaji mzuri wa shughuli za maendeleo hususani ukusanyaji wa mapato ya ndani ambapo kwa miaka 3 mfululizo imeongoza kwa ukusanyaji mapato uliovuka malengo ya mwaka kwa mkoa wa Kagera, na hapa nitoe malekezo mahususi kwa harmashauri nyingine kuiga mfano huu.” alieleza Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti.

Mkuu wa mkoa Kagera akiwahuitubia wavuvi pamoja na wananchi katika kijiji cha katembe Kata Nyakabango wilayani Muleba wakati wa hafla ya kukabithi Boti.


Gaguti amewataka watendaji waliokabithiwa boti hizo kuhakikisha wanazifanyia kazi iliyokusudiwa na kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi maana hakuna tena visingizio vya kwenda kuwahudumia wananchi kwa kigezo cha usafiri, na kuwasihi kutozitumia kama fimbo ya kuwanyanyasa wananchi badala ya kuwahudumia.

Aidha, amewasihi wananchi kuanza kujishughulisha na uvuvi wa kisasa kwa kuwa na vikundi vitakavyowawezesha kupata fedha kutoka taasisi za kifedha Pia watumie zana za kisasa na kuwa malengo ya kufanya uvuvi wa kibiashara hata kwa nje ya nchi na kueleza kuwa mkoa umejipanga kuleta wawekezaji watakaowekeza katika sekta ya uvuvi.

“Tunatakiwa kujua kuwa Mkoa wa Kagera ni mkoa wa kimkakati kwa maendeleo ya nchi, sisi kama Serikali ya mkoa tunao mpango wa kuwaleta wawekezaji watakao wekeza katika sekta ya uvuvi hivyo ni wasihi wananchi na wavuvi tufanye uvuvi wa tija wenye kufata taratibu zote kwa kutumia nyezo zinazoruhusiwa, tutakuwa waajabu kama tutawaleta wawekezaji na tukakutwa sisi wazawa ndo sababu ya kubwa ya kuendeleza uvuvi haramu katika ziwa letu.” Alisisitiza Gaguti.


Ad
Ad

Unaweza kuangalia pia

Tanzania Yapiga Hatua Kubwa katika Miradi ya Maji, Zaidi ya Miradi 1,500 Yakamilika Vijijini na Mijini.

Tanzania imefanya maendeleo makubwa katika miradi ya maji, na hadi sasa, miradi mingi imekamilika ili …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *