RAIS MAGUFULI ATEMBELEA MSIKITI MKUU KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 13 Oktoba, 2020 ametembelea Msikiti Mkuu uliojengwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam kwa ufadhili wa Mfalme Mohammed VI wa Morocco.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Bin Ally, Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane wakati alipotembelea Msikiti Mkuu wa BAKWATA uliopo Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam ambao umekamilika kujengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed VI wa Morocco wakati akielekea Mburahati kwa ajili ya Mikutano ya Kampeni za Urais kwa upande wa Chama cha Mapinduzi CCM leo tarehe 13 Oktoba 2020.

Msikitini hapo, Mhe. Rais Magufuli amepokelewa na Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zuberi Ally, Balozi wa Morocco hapa nchini Mhe. Abdelilah Benryane na viongozi wengine wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) ngazi ya Taifa na Mkoa wa Dar es Salaam.

Ad
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo wakati alipotembelea Msikiti Mkuu wa BAKWATA uliopo Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam ambao umekamilika kujengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed VI wa Morocco baada ya Mhe. Rais Magufuli kumuomba Mfalme wa Morocco kuwajengea Waislamu Msikiti alipofanya ziara hapa nchini tarehe 24 Oktoba, 2017

Ujenzi wa Msikiti huo ulioanza mwaka 2019 baada ya Mhe. Rais Magufuli kumuomba Mfalme Mohammed VI (aliyekuwa katika ziara ya Kitaifa hapa nchini) ajenge Msikiti mkubwa kwa ajili ya Waislamu wa Tanzania, umekamilika kwa asilimia 100 na hivi sasa unasubiri kuzinduliwa rasmi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane wakati alipokuwa akielezea ujenzi huo wa Msikiti mpya uliokamilika kujengwa katika Makao makuu ya Bakwata Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuutembelea na kujionea ukiwa umekamilika, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na ubora wa hali ya juu wa Msikiti huo, jinsi unavyovutia na amesema ameridhishwa na kazi kubwa iliyofanywa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Bin Ally, Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane wakati alipotembelea Msikiti Mkuu wa BAKWATA uliopo Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam ambao umekamilika kujengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed VI wa Morocco wakati akielekea Mburahati kwa ajili ya Mikutano ya Kampeni za Urais kwa upande wa Chama cha Mapinduzi CCM leo tarehe 13 Oktoba 2020.

Mhe. Rais Magufuli ameahidi kuandika barua ya kumualika Mfalme Mohammed VI kuja hapa nchini kuzindua Msikiti huo kama alivyoahidi na amemuomba Balozi wa Morocco hapa nchini Mhe. Benryane kutanguliza salamu zake za shukrani kufuatia kukamilika kwa ujenzi huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa Dua iliyokuwa ikiongozwa Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Bin Ally mara baada ya kutembelea Msikiti Mkuu wa Bakwata uliokamilika kujengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed VI wa Morocco.

Wakiwa Msikitini hapo, Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zuberi Ally ameomba dua kwa ajili ya Taifa, amemuombea Mhe. Rais Magufuli, na pia shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kufanikisha ujenzi wa Msikiti huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Bin Ally, Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane wakwanza kushoto, pamoja na viongozi mbalimbali wa Bakwata mara baada ya kutembelea Msikiti Mkuu wa Bakwata uliokamilika kujengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed VI wa Morocco. PICHA NA IKULU
Ad

Unaweza kuangalia pia

Mkutano wa Tatu wa Jukwaa la Haki za Watoto

Tarehe 4 hadi 5 Aprili 2024, umefanyika Mkutano wa Tatu wa Jukwaa la Haki za …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *