SERIKALI IMEJIPANGA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAWEKEZAJI

Ikiwa ni wiki moja baada Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa kutoa maagizo kwa Wizara ya Viwanda na Biashara kufika kwenye kiwanda cha maziwa kinachojegwa kihanga, Wilayani Karagwe ili kutatua changamoto anazozipata Mwekezaji wa kiwanda hicho.

Oktoba 12,2020 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Ludovick Nduhiye amefika eneo kinapojejwa kiwanda cha kuchakata maziwa cha Kahama Fresh kinachojengwa eneo maalum la viwanda lililopo Kihanga, wilaya ya Karagwe, Mkoa Kagera.

Ad

Ujio wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara umekuwa na lengo la kukagua na kufuatilia  utekelezaji wa maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na kutatuliwa kwa baadhi ya changomoto ambazo mwekezaji amekuwa akikabiliana nazo katika ujenzi wa kiwanda hicho.

Mkurugenzi wa Kahama Fresh, Jossam Ntangeki (kushoto) akitoa maelezo ya ujenzi wa kiwanda kuchakata maziwa cha Kahama Fresh kitakachokuwa na uwezo wa kuchakata Lita 10,000 kwa mzunguko mmoja kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Ludovick Nduhiye, Kulia ni Mkurugenzi msaidizi wa EPZA, James Maziku. Kihanga, Karagwe. Oktoba 12,2020 

“Nimakuja kufuatilia yale tuliyokubaliana mwezi wa sita nilipokuja karagwe, tulikubaliana eneo hili kuwa eneo maalum la uwekezaji kiuchumi (special economic zone) chini ya EPZA lakini eneo hili tutaliunganisha na eneo la Rukombe, Chamchuzi ili kuhakikisha tunawavutia wawekezaji wa ndani na nje maana uwekezaji unaofanywa hapa na ndugu Jossam ni mfano wa kuigwa’’ Amesema Nduhiye

Nduhiye amepongeza jitihada za mwekezaji mzawa wa Kahama Fresh Limited, Bwana Jossam Ntangeki kwa hatua waliyofikia katika ujenzi wa kiwanda cha maziwa na kusaidia utekelezaji wa dira ya Serikali ya awamu ya tano katika ujenzi wa uchumi wa viwanda maana kwa mkoa hapakuwa na kiwanda cha maziwa chenye ukubwa wa kuchakata lita 10,000 kwa siku na amepongeza uwepo wa pango wa ujenzi wa kiwanda kinachotengeneza vyakula vya ng’ombe wa maziwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Karagwe, Godwin Kitonka ametoa ufafanuzi wa mpango wa kutangaza eneo hilo kuwa eneo maalum la uwekezaji wa viwanda kwa wilaya karagwe na akatoa takwimu ya  zoezi la kugawa ngo’ombe kwa wafugaji wadogo wadogo ambapo mpaka sasa wametolewa ng’ombe 300 ambao itasaidia upatikanaji wa malighafi ya maziwa kwa ajili ya kiwanda hicho.

Eneo unapofanyika ujenzi wa kiwanda cha kuchakata maziwa cha Kahama Fresh kitakachokuwa na uwezo wa kuchakata Lita 10,000 kwa mzunguko mmoja na gharama za ujezi mpaka kukamilika ni Billioni 2.4, kinachojengwa eneo maalum la viwanda lililopo Kihanga, wilaya ya Karagwe, Mkoa Kagera. Oktoba 12,2020

Nae Mkurugenzi wa kampuni ya Kahama Fresh Limited, Jossam Ntangeki ameishukuru Serikali kuendelea kutatua changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo pia ameshukuru wizara kwa kuwawekeaa mazingira mazuri ya uwekezaji kwa kutenga maeneo maalum ya viwanda kwa kila wilaya na kuwasogezea mahitaji muhimu ambayo yanahitajika katika uwekezaji wao.

Jossam wakati akitoa taarifa ya kiwanda kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara amesema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho umefikia kiwango cha kujenga majengo ya ofisi na kusawazisha eneo kitakapojegwa kiwanda na amesema kiwanda kitakamilika ndani ya miezi sita na kitakuwa na uwezo wa kuchakata Lita 10,000 kwa mzunguko mmoja na gharama za ujezi mpaka kukamilika ni Billioni 2.4  ambapo kwa sasa kampuni imeajiri wafanyakazi 104 na madakitakitari wa mifugo watano.

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *