SERIKALI KUTUMIA BILIONI 1 KUTATUA CHANGAMOTO YA HUDUMA YA MAJI JIJINI DODOMA

Serikali kupitia Wizara ya Maji imeipatia Mamlaka ya Majisafi na Usafi waMazingira Mjini Dodoma (DUWASA) kiasi cha shilingi bilioni 1 iii kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo yenye changamoto ya huduma hiyo jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga alipotembelea kisima kimojawapo kati ya visima vinavyochimbwa katika eneo la lhumwa jijini Dodoma.

Ad

“Hili linafanyika kutokana na ongezeko la mahitaji ya huduma ya maji katika maeneo mbalimbaji ya jiji la Dodoma hasa maeneo ya pembezoni” Mhandisi Sanga amesema.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Bilinith Mahenge akiwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga wakiangalia kazi inavyoendelea

Aidha, amefafanua kuwa kuhamia kwa Serikali jijini Dodoma ni fursa kwa taasisi za maji zilizoko Dodoma kutatua changamoto za huduma ya maji wanazozipata wananchi wa Dodoma.

Mhandisi Sanga amongeza kuwa Serikali ina mipango ya muda mfupi, ya kati na ya muda mrefu ya kutatua changamoto za upatikanaji wa huduma ya maji.

“Mipango ya muda mfupi ni kama ujenzi wa visima vya dharula katika eneo la lhumwa na mipango ya muda wa kati ni ujenzi wa bwawa la Farkwa na muda mrefu ni kutoa maji kutoka ziwa Victoria” amefafanua Mhandisi Sanga.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi David Pallangyo ameongeza kuwa ujenzi wa kisima hicho eneo la lhumwa ni mojawapo ya visima kadhaa vitakavyoweza kuzalisha maji na kuyatoa kuyapeleka hadi mjini iii kupunguza tatizo la maji eneo la mjini.

“Vitachimbwa visima vinavyozalisha si chini ya mita za ujazo elfu tatu kwasiku zitakazosaidia kupunguza tatizo la maji maeneo ya pembezoni kama Mwangaza, Njedengwa, lhumwa na maeneo mengine ya mjini.
Mhandisi Pallyangyo amesema mradi wa ujenzi wa visima eneo la lhumwa utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.4.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge ameupongeza uongozi wa DUWASA kwa kutatua changamoto za maji jijini Dodoma na kuwataka kuongeza ushirikiano iii kufikia malengo

Lengo la juhudi zote za Serikali ni kuhakikisha huduma ya majisafi na uondoshaji wa majitaka zinakuwa za uhakika zinazoendana na hadhi ya jiji la Dodoma ambalo ndio makuu ya nchi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *