HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI YA KWANZA KWA UBORA AFRIKA 2020

Hifadhi ya Taifa Serengeti imeshinda Tuzo ya kuwa Hifadhi Bora katika Bara la Afrika kwa mwaka 2020. Tuzo hiyo imetangazwa Novemba 9,2020 na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) ya nchini Marekanl kwa njia ya Mtandao.


Hii ni mara ya pili kwa Hifadhi ya Taita Serengeti kushinda katika Kundi la Hifadhi zinazoongoza kwa ubora zaidi Bara la Afrika baada kushinda pia mwaka 2019.

Ad


Serengeti imeibuka na ushindi katika shindano hilo lililoshindanisha hifadhi nyingine za Central Kalahari (Botswana); Etosha (Namibia); Kidepo Valley (Uganda): Kruger (Afiika ya Kusinl) na Maasai Mara National Reserve (Kenya).


Serengeti inajivnia umaarufu wa msafara wa nyumbu wahamao zaaidi ya milioni moja na nusu, aina mbalimbali za wanyamapori wanaopatikana kwa wingi.

Mandhari nzuri ya kuvutia pamoja na shughuli mbalimball za utalli zinazovutia watalli wengi. Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wananchi, Wadau wa Utali pamoja na wale wote waliotumia muda wao kupiga kura na kuifanya Serengeti kuwa mshindi wa Hifadhi Bora zaidi kwa Bara la Afrika kwa mwaka 2020.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *