MIRADI YA MAJI CHALINZE INATARAJIWA KUKAMILIKA MWAKA 2021

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete akizungumza na Meneja DAWASA – Chalinze, Bw. Onest Makoi

Meneja wa Dawasa wa Chalinze mkoani Pwani amesema kuwa miradi maji inayoendelea katika jimbo la Chalinze inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Mwaka 2021.

Amezungumza hayo wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ya kukagua miradi ya maji inayoendelea.

Ad

Meneja huyo wa DAWASA amesema kuwa wananchi wawe tayari kwa maboresho yanayofanywa ikiwemo upanuzi wa miundombinu ya maji, umaliziaji wa Ujenzi wa Matenki na usambazaji awamu ya Tatu.

Ambapo ameeleza kuhusu ujenzi wa mradi wa Ruvu – Mboga ambao ununuzi wa Vifaa kwa ajili ya ujenzi uko hatua ya Mwisho.

Kwa upande wa Mh. Mbunge Ridhiwani Kikwete aliwashukuru Dawasa kwa hatua kubwa wanazoendelea kufanya na kumshukuru Raisi Dkt. John Magufuli kwa kuendelea kuwaangalia wananchi wa Chalinze kwa kuendelea kutatua kero mbalimbali ikiwemo za maji.

Ridhiwani Kikwete anafanya ziara jimboni humo ya kutembelea miradi ya huduma za jamii inayoendelea ambapo pia atatembelea Ofisi za TARURA kujua hali ya maandalizi ya marekebisho ya Miundombinu ya barabara vijijini na mijini.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Askofu Dkt Maasa OleGabriel RAIS SAMIA ANATEKELEZA MAAGIZO YA MUNGU YA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI

Askofu Dkt. Maasa OleGabriel Katibu Mkuu Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania na Askofu wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *