TANZANIA YAWASILISHA OMBI MAALUM AU

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja Jamhuri ya Afrika Kusini zimewasilisha ombi maalumu kwa Umoja wa Afrika kuzitambua rasmi njia zilizotumika na wapigania uhuru kutoka Dar es Salaam kupitia nchi mbalimbali Kusini Mwa Bara la Afrika hadi Namibia kuwa urithi wa Kimataifa.

Ombi hilo limewasilishwa na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa katika Mkutano wa 34 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika unaofanyika kwa njia mtandao na kuungwa mkono na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi ambaye alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli. 

Pia Tanzania imeuomba Umoja wa Afrika kuitambua lugha ya Kiswahili kama lugha ya asili na ya ukombozi katika Bara la Afrika kwa kuwa ndiyo lugha iliyotumika kwa ajili ya mawasiliano na mafunzo kwa wapigania uhuru ikizingatiwa kuwa kauli mbiu ni sanaa,utamaduni na urithi.

Akiufunga Mkutano huo wa siku mbili, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Felix Tshisekedi amesisitiza kuwa umoja, mshikamano na amani katika bara la Afrika ndiyo nyenzo pekee itakayoliwezesha bara hilo kuendelea kiuchumi ili kuendana na rasilimali ilizonazo.

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.