JAJI IMANI ABOUD APENDEKEZWA KUGOMBEA URAIS WA MAHAKAMA YA AFRIKA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Jaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kutoka Tanzania Mhe. Jaji Imani Aboud katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Jaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kutoka Tanzania Jaji Imani Aboud amependekezwa kugombea Urais wa Mahakama hiyo.

Jaji Aboud amesema endapo atashinda katika nafasi hiyo na kuibuka mshindi itakuwa ni heshma kubwa kwa nchi na kwake mwenyewe kushika wadhifa mkubwa katika mahakama ya Afrika kuhusu masula ya haki za binadamu

Ad

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema Tanzania inayo imani na Jaji Imani Aboud kwa kuwa ana uzoefu mkubwa katika masula ya kimahakama hivyo ushindi wake utakuwa ni sifa kwa Taifa na kwa wanawake kuendelea kushika nyadhifa kubwa sio Serikalini tu, bali kwenye taasisi na mashirika ya kimataifa.

Majaji wengine wanaogombea nafasi hiyo ni kutoka katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Malawi na Cameroon ambapo Hayati Jaji Augustino Ramadhani ndie alikuwa Mtanzania wa mwisho kushika nafasi hiyo ya Urais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *