WAZIRI AWESO AITUMIA BASHUNGWA CUP KUWAPA MBINU WABUNGE

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ametoa rai kwa wabunge hapa nchini kuziomba  mamlaka zinazowazunguka  kuboresh miundombinu ya  michezo ikiwa ni pamoja na viwanja vya michezo katika maeneo yao ili kuwa katika viwango vinavyotakiwa.

 Mhe. Aweso amefafanua kwamba  endapo viwanja vya michezo vitakuwa katika viwango vinavyotakiwa, hali hiyo itawafanya vijana wengi kushawishika  kushiriki michezo mbalimbali.

Ad

Rai hizo  amezitoa  jana (Septemba 12) wakati akihitimisha ligi ya Bashungwa Cup iliyokuwa ikizishirikisha timu 23 kutoka kata 23 za Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso na mgeni rasmi katika kilele cha mashindano ya Bashungwa CUP 2021 akimkabidhi kombe mwakilishi wa timu ya Bugeni FC baada ya kuibuka washindi kwa mikwaju ya pemaliti dhidi ya washindani wao FC katika fainali za Bashungwa Cup 2021.

Kauli ya Waziri Aweso inafutia ombi la wakazi wa wilaya ya Karagwe waliozungumza kwa nyakati tofauti tofauti wakiomba Halmashauri ya wilaya hiyo kuufanyia ukarabati uwanja wa mpira wa Kayanga ili uwe na viwango vya kuruhusu mashindano makubwa ya ngazi ya mkoa na hata taifa kufanyika uwanjani hapo.

Akizungumza katika fainali hizo mwandaaji wa mashindano hayo ambaye ni mbunge wa Jimbo la Karagwe na Waziri anayesimamia sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono jitihada za kukuza michezo katika safari ya kukuza vipaji vya vijana.

“Wote tunaamini kwenye umoja, ninamaanisha tukiungana tunaweza, Serikali inafanya kila kinachowezekana kukuza sekta ya michezo nchini, lakini si dhambi kwa mdau yeyote kutuunga mkono popote unapoweza katika kutimiza ndoto ya vijana wetu wenye vipaji vya michezo.” Alisema Waziri Bashungwa.

 Fainali hiyo iliyozikutanisha timu mbili ambazo ni Bugeni FC na Nyabiyonza FC zote za wilayani Karagwe. Timu ya Bugeni FC imeibuka mshindi kwa mikwaju ya penaliti na kubeba kombe pamoja na zawadi ya shilingi milioni mbili na laki tano huku timu ya Nyabiyonza ikishika nafasi ya pili na kubeba kitita cha shilingi milioni moja laki mbili na elfu 50, huku mshindi wa tatu ambaye ni Kihanga FC akiibuka na shilingi laki saba na elfu hamsini.

Mashindano ya Bashungwa Cup yalizinduliwa rasmi mwaka 2017 na yamekuwa yakiwakutanisha vijana kila mwaka kushindania zawadi mbalimbali, lengo likiwa ni kuwaunganisha wakazi wa wilaya ya Karagwe na kuibua vipaji vya vijana kupitia mchezo wa soka.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *