KONGAMANO LA WADAU KUHUSU UPATIKANAJI WA RASILIMALI ZA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI LAZINDULIWA

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akiteta jambo na Mkurugenzi wa REPOA Dkt. Donald Mmari (kushoto) mara baada ya kufungua Kongamano la Wadau wa Kitaifa kuhusu upatikanaji wa Rasilimali za kusaidia utekelezaji wa Mikakati ya Taifa ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi hii leo katika ukumbi wa Royal Village Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew Komba.
Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar akizungumza na Bw. Richard Muyungi ambaye ni Mjumbe wa Green Climate Fund kwa niaba ya Afrika, kuhusu Maandalizi ya Mkutano wa Glasgow hasa matarajio ya Afrika na Tanzania katika Mkutano huo kuhusu upatikanaji wa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.
Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar akihutubia wadau walioshiriki kongamano la Kitaifa kuhusu upatikanaji wa Rasilimali za kusaidia utekelezaji wa Mikakati ya Taifa ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi. Mhe. Balozi amesisitiza kuendelea kushirikiana na Tanzania katika jitihada za kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabianchi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akifungua Kongamano la Wadau wa Kitaifa kuhusu upatikanaji wa Rasilimali za kusaidia utekelezaji wa Mikakati ya Taifa ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi. Kongamano hilo limefanyika hii leo 23/09/2021 katika Ukumbi wa Royal Village Dodoma. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew Komba, Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar na Mkurugenzi wa REPOA Dkt. Donald Mmari.
Ad

Unaweza kuangalia pia

Uzinduzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya UCSAF Dodoma: Kuimarisha Mawasiliano Vijijini

25 Aprili 2024, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *