RAIS SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI NGO’S NA AONGOZA WATANZANIA KUAGA MWILI WA OLE NASHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha Taarifa ya Kielektroniki ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali NGO’s kwa maendeleo ya Taifa katika mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) uliofanyika leo Sept 30,2021 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijji Dodoma.

Rais Samia Suluhu Hassan, ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuongeza uwazi na uwajibikaji katika kazi zao pamoja na kwenda sambamba na vipaumbele na mipango ya Serikali ili ziweze kuleta tija katika jamii.

Mhe. Rais Samia amesema hayo leo tarehe 30 Septemba, 2021 wakati akihutubia katika Mkutano wa Mwaka wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa  Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Ad

Mhe. Rais Samia amesema kwa sasa Serikali inatekeleza Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021/2026) hivyo ni vyema Mashirika hayo kuandaa mipango yake kwa kuoanisha na mpango huo wa Serikali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijji Dodoma leo Sept 30,2021.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akimkabidhi Tuzo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kutambua kazi kubwa anayoifanya katika kujenga Taifa la Tanzania, kwenye mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) uliofanyika leo Sept 30,2021 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijji Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kazi za Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) alipotembelea mabanda ya maonesho katika mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) uliofanyika leo Sept 30,2021 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijji Dodoma.

Aidha, Rais Samia ameyataka Mashirika hayo Yasiyo ya Kiserikali hususan ya ndani pamoja na Wizara husika kuandaa mpango mkakati utakaosaidia Mashirika hayo kuondokana na utegemezi katika utendaji wa kazi zao.

Mhe. Rais Samia ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kufanya kazi zinazoendana na mila, utamaduni, desturi na maadili ya kitanzania pamoja na kusimamia sheria zinazoongoza Mashirika hayo.

Vilevile, Mhe. Rais Samia ameyaomba Mashirika hayo kufanya kazi pamoja na Serikali katika kuwaelimisha wananchi kuhusu kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika Agosti 2022, na kuwapa wananchi elimu ya tahadhari za kujikinga na UVIKO 19.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu na Uwekezaji Hayati William Tate Ole Nasha wakati wa kuaga mwili wa Naibu Waziri huyo katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo Sept 30,2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Watanzania kuaga mwili wa aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu na Uwekezaji Hayati William Tate Ole Nasha katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo Sept 30,2021

Katika mkutano huo, Mhe. Rais Samia amezindua Taarifa ya mchango wa Mashirika hayo Yasiyo ya Kiserikali katika maendeleo ya Taifa.

Wakati huohuo, Mhe. Rais Samia, ameongoza waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Marehemu William Tate Ole Nasha.

Shughuli za kuaga mwili wa Marehemu Ole Nasha zimefanyika katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Daniel Chongolo, Mawaziri na Manaibu Mawaziri, Wabunge pamoja na viongozi wengine wa  vyama vya Siasa na Serikali.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Uzinduzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya UCSAF Dodoma: Kuimarisha Mawasiliano Vijijini

25 Aprili 2024, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *