Mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya nje wa Nchi za Afrika na Nordic (Afrika 29 na 5 za Nordic)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli amefungua Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya nje wa Afrika-Nordic jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa JNICC.

Mada ya mkutano wa mwaka huu Ushirikiano kwa maendeleo endelevu.

Ad

Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiaano wa Kimataifa Profesa Palamagamba Kabudi amewaalika wenzake kadhaa wa Kiafrika na Nordic kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya nje wa Afrika-Nordic jijini Dar es salaam tarehe 8 Novemba, 2019.

Mkutano huo umehudhuriwa na mawaziri 29 wa kigeni wa nchi za Afrika na wengine watano kutoka nchi za Nordic ambazo ni Swiden, Denmark, Finland, Norway na Iceland.

Nchi za Afrika ambazo zimehudhuria mkutano huu ni Algeria, Angola, Benin, Botswana, Burkinafaso, Burundi, Comoros, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Misri, Ethiopia na Ghana.

Nchi zingine ni; Kenya, Lesotho, Mali, Malawi, Moroko, Msumbiji, Namibia, Nigeria, Niger, Rwanda, Senegal, Somalia, Afrika Kusini, Tunisia, Uganda, Zambia, Zimbabwe na mwenyeji -Tanzania.

Mbali na mawaziri wa mambo ya nje mkutano huo pia umehudhuriwa na mabalozi wa nchi zinazoshiriki za Kiafrika na Kutoka katika nchi za Nordic.

Ushirikiano kwa Maendeleo Endelevu.

Screen Shot 2019-11-08 at 10.47.07.png

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Taasisi ya Huduma za Afya Aga Khan, Mwana Mfalme Bi. Zahra Aga Khan

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *