Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeagiza mitambo mitatu ya uchorongaji yenye teknolojia ya kisasa zaidi kuwahi kutumika hapa nchini, ambapo mmoja wa mtambo huu unauwezo wa kuendeshwa kwa kutumia computer na mtu akiwa mbali na mashine
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof Simon Msanjila katika uzinduzi wa mitambo hiyo, na kuipongeza STAMICO kwa hatua waliofikia na uthubutu wa kuleta ushindani katika soko la uchorongaji amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidi ili kuleta tija na maendeleo kwa Taifa
Msanjila amesema kuwa Shirika limethubutu na limedhamiria kuleta mapinduzi katika soko la madini kwa kuingia kwa nguvu zote kwenye shughuli za uchorongaji.