Matokeo ChanyA+

Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+.

BALOZI WRIGHT – MAREKANI INAIONA TANZANIA NI NCHI IMARA, TULIVU NA YENYE DEMOKRASIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 02 Agosti, 2020 amepokea Hati za Utambulisho za Mabalozi 2 walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa Tanzania. Balozi wa Marekani hapa nchini Donald John Wright akiwa amesimama wakati nyimbo za Mataifa mawili ya Tanzania na Marekani zilipokuwa zikipigwa na …

Soma zaidi »

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MAONESHO YA NANENANE MKOANI SIMIYU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akilihutubia Taifa kwenye Sherehe ya Uzinduzi  wa Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane Kitaifa katika Viwanja  vya Nyakabindi Mkoani Simiyu leo Agosti 01,2020. ambapo ujumbe wa mwaka huu Nanenane kwa maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Kiongozi …

Soma zaidi »

TUHAKIKISHE UCHAGUZI WA MWAKA HUU UNAKUWA WA AMANI NA UTULIVU -WAZIRI MKUU MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kila Mtanzania anapaswa kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu unakuwa wa amani na utulivu. Amesema kuwa kiongozi wa nchi, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa uchaguzi utakuwa wa huru na haki. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Julai 31, 2020) wakati akishiriki swala na …

Soma zaidi »

RAIS DKT. MAGUFULI ACHANGIA SHILINGI MILIONI TANO KWA SHULE YA MSINGI SOMANGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Jogoo alilopewa na Mzee Shaweji Mohamed Kimbwembwe mkazi wa Somanga mkoani Lindi ambaye alifurahishwa na utendaji kazi wa Mhe. Rais Magufuli wa kuwaletea maendeleo Wananchi wanyonge Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John …

Soma zaidi »

RAIS DKT. MAGUFULI AKIPITA KWENYE DARAJA LA MKAPA RUFIJI MKOANI PWANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipita na kukagua Daraja la Mkapa linalopita katika Mto Rufiji mkoani Pwani wakati akitokea Masasi Mtwara kwenye msiba wa Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa leo tarehe 30 Julai 2020. Daraja hilo linalounganisha Pwani …

Soma zaidi »

WAZIRI WA UJENZI AJIPANGE VIZURI NAMNA YA KUTAFUTA UTATUZI WA BARABARA HII – RAIS DKT. MAGUFULI

Alichozungumza Rais Dkt. John Magufuli aliposimama kuongea na wananchi wa Nangurukuru Mkoani Lindi akiwa njiani akitokea mkoani Mtwara. “Lakini nimeamua kupitia barabara hii nilitakiwa niende na ndege nikasema hapana najua wasaidizi wangu watashangaa kuona badala ya kwenda Airport Mtwara niende na ndege nilitaka nipite hii barabara nione hali yake” “Hii …

Soma zaidi »

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUFUNGUA MAONYESHO YA NANE MKOANI SIMIYU

Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Bwana Gerald Kusaya mapema tarehe 29 Julai, 2020 ametembelea Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu na baadae alielekea katika Viwanja vya Nyakabindi. Katibu Mkuu Kusaya aliekea katika Viwanja vya Nyakabindi ili kujionea na kukagua maandalizi ya eneo la maonyesho ikiwa ni pamoja na kujionea …

Soma zaidi »

KATIBU MKUU KILIMO KUSAYA AGAWA PIKIPIKI 18 KWA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI NCHINI

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya amesema kuwa serikali imeendelea kuboresha sekta ya kilimo kwa kutoa Dola Milioni 35.3 kwa ajili ya kuwezesha mapambano dhidi ya Sumukuvu katika mazao ya wakulima nchini. Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma wakati wa kutoa pikipiki kwa wakurugenzi wa halmashauri 18 wa Tanzania bara kwa …

Soma zaidi »

WANANCHI WAMESHAURIWA KUJENGA TABIA YA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA

Wananchi wameshauriwa kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara kwa kufanya hivyo watatambua kama wana maradhi au la na kama wana maradhi wataweza  kupata huduma za matibabu kwa wakati. Pia wameombwa kuwa na bima ya afya ambazo zitawasaidia kupata matibabu pindi watakapouguwa  kwani maradhi huja muda wowote, wakati …

Soma zaidi »