WAZIRI WA UJENZI AJIPANGE VIZURI NAMNA YA KUTAFUTA UTATUZI WA BARABARA HII – RAIS DKT. MAGUFULI

Alichozungumza Rais Dkt. John Magufuli aliposimama kuongea na wananchi wa Nangurukuru Mkoani Lindi akiwa njiani akitokea mkoani Mtwara.

“Lakini nimeamua kupitia barabara hii nilitakiwa niende na ndege nikasema hapana najua wasaidizi wangu watashangaa kuona badala ya kwenda Airport Mtwara niende na ndege nilitaka nipite hii barabara nione hali yake”

Ad

“Hii barabara imeharibika huwezi kuamini kama tuna Waziri wa Ujenzi au Naibu Waziri wa ujenzi au Katibu Mkuu wa Wizara ya ujenzi au Chief Executive wa Tanroads au Regional Manager wa Mkoa wa Lindi kwasababu kilometa zote 90 nilikuwa nazihesabu zimeharibika”

“Na walioharibu hii barabara nataka niseme ukweli ni Wizara ya ujenzi kwasababu wameruhusu magari mazito yanayobeba gypsum yale ya mawe kuharibu barabara yetu ninawapa pole sana ngoja niende ofisini ninakwenda kushugulikia suala la kutatua utatuzi wa barabara hii”

“Tukiiacha katika hali hii itaendelea kuleta ajali lakini tutarudi kule tulikotoka kwahiyo ndugu zangu wasafiri nimeona nilizungumze hili, ndugu zangu wa Nangurukuru nimeona nilizungumze hili nimefanya vizuri kupitia hii barabara kwasababu nisingepita wangenidanganya”

“Sio barabara niliyoiacha nikiwa Waziri wa ujenzi sio hii barabara ambayo imeanza kuharibika, imebonyea kila maeneo, kwahiyo utunzaji wa Wizara ya ujenzi uko weak nina uakika kwa maneno haya Waziri wa ujenzi ajipange vizuri namna ya kutafuta utatuzi wa barabara hii”

“Ndugu zangu wa safari endeleeni kuiamini Serikali yenu tupo pamoja kwa raha kwa shida tupo pamoja nimetoka kule Masasi palikuwa na madeni ambayo yalikuwa yamebaki ya kulipa wakulima wa korosho tumeshatoa bilioni 20 kwahiyo hakuna mkulima yoyote wa korosho atakaye dai deni na Serikali tumemaliza huo mzizi wa fitna, bilioni 20 zilitoka kuanzia wiki iliyopita kwahiyo wale ambao hawakupata sifahamu lakini mimi najua wanaendelea kulipwa maeneo haya yote walikuwa wanadai korosho tumetoa bilioni 20 ili kutatua kero za wananchi walikuwa bado wanadai”

“Tumeshalipa hela zaidi ya bilioni 800 kwa ajili ya korosho tumemalizia na hizi bilioni 20 zilizobaki kwahiyo ndugu zangu watanzania, ndugu zangu wa Kusuni tuendelee kushikamana na Serikali yetu, tuendelee kumtanguliza Mungu mbele, tuendelee kuchapa kazi” – Rais Dkt. John Magufuli

Ad

Unaweza kuangalia pia

Na Haya Ni Maboresho Makubwa katika Sekta ya Afya Nchini Tanzania

Nchi yetu inajivunia hatua kubwa tunazoendelea kupiga kwenye eneo hili ambapo pamoja na maboresho na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *