MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUFUNGUA MAONYESHO YA NANE MKOANI SIMIYU

Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Bwana Gerald Kusaya mapema tarehe 29 Julai, 2020 ametembelea Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu na baadae alielekea katika Viwanja vya Nyakabindi.

Katibu Mkuu Kusaya aliekea katika Viwanja vya Nyakabindi ili kujionea na kukagua maandalizi ya eneo la maonyesho ikiwa ni pamoja na kujionea jengo la Wizara ya Kilimo ambalo litakuwa sehemu ya kutolea mafunzo ya kudumu kwa Wakulima wa Mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara.

Ad

Awali katika mazungumzo yake na Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Bwana Ekwabi Mujungu amemweleza Katibu Mkuu Kusaya kuwa maandalizi kwa upande wa mkoa wa Simiyu na Halmashauri zake yanaendelea vizuri.

“Tarehe 1 Agosti, 2020 tunataraji; Mgeni wetu Rasmi; atakuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ambaye atafungua rasmi Maadhimisho ya mwaka huu na baadae Rais wa Awamu ya Tano, Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli atahitimisha; Nawakaribisha Wananchi wote.” Katibu Mkuu Kusaya

Ad

Unaweza kuangalia pia

KWA MARA YA KWANZA WATAALAMU WAZAWA WAZIBUA MISHIPA PACHA YA MOYO ILIYOZIBA KWA ASILIMIA 95

Kwa mara ya kwanza wataalamu wazawa wa magonjwa ya moyo na wazibuaji wa mishipa ya …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.