Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Rukia Muwango atangaza uzinduzi wa msibu wa mauzo ya korosho wilayani humo.

NACHINGWEA YATANGAZA UZINDUZI WA MSIMU WA UUZAJI KOROSHO 2018/2019

MKUU WA WILAYA YA NACHINGWEA MKOANI LINDI, MHE. RUKIA MUWANGO
Mhe. Rukia Muwango ametangaza kuwa siku ya Jumamosi ya tarehe 13 Oktoba, 2018 kuwa ni siku ya uzinduzi wa uuzaji wa korosho wilayani humo.

Pamoja na uzinduzi huo, Mhe. Rukia ameendelea kuunga mkono wito wa serikali kwa kukaribisha wawekezaji wa viwanda vya kubangua korosho wilaya humo ili wakulima wanufaike zaidi na kuongeza thamani ya zao hilo sambamba ya ajira kwa wakulima na watakao ajiriwa katika viwanda vhivyo.

KOROSHO GHAFI KABLA YA KUU
Korosho ghafi kabla kubanguliwa ikiwa tayari kupimwa na kupelekwa sokoni kuuzwa. Serikali ya Tanzania bado inasisitiza uzaji wa korosho iliyobanguliwa ili kuongeza thamani ya zao hilo na kumnufaisha mkulima kwa kiwango kinachostahili. Mhe. Rais Magufuli, kupitia wizara ya Kilimo na wizara ya Viwanda na Biashara imeweka mikakati na mazingira mazuri ya uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo, vya kati na vikubwa vya kubangua korosho kabla ya kuuzwa kwenye soko la nje ya nchi.
  • Tarehe ya Uzinduzi 13/10/2018 siku ya Jumamosi
  • Uzinduzi kufanyika MNERO NGONGO
  • Utaanza saa tatu asubuhi (09:00 AM)
DC-NACHINGWEA-1.png
Pichani, Mheshimiwa Rukia Muwango akiwa na baadhi ya viongozi wilayani humo katika maandalizi ya uzinduzi wa msimu wa uuzaji wa korosho siku ya Jumamosi tarehe 13/10/2018.

Sambamba na uzinduzi huo, kutakuwa na utaratibu wa mambo kadhaa ili kufanikisha uzaaji korosho bora na wenye tija kwa mkulima;

Ad
  • Kutatolewa elimu ya mauzo ya korosho kwa mfumo wa Stakabadhi ghalani

WAKULIMA WA KOROSHO BAADA YA KUVUNA KOROSHO

  • Mwongozo wa Mauzo ya korosho
  • Kutatolewa elimu na maelekezo ya masuala ya kibenki.
  • Viongozi wa serikali watakuwepo kwaajili ya kutoa maelekezo rasmi ya serikali kuhusu biashara ya korosho nchini.
ZAO LA KOROSHO
Koshosho ya Tanzania inafahamika kama DHAHABU YA MTINI kutokana na ubora wake.
  • Wataalam wa afya watakuwepo ili kuongoza wakulima na wafanyabiashara wa korosho katika zoezi la upimaji afya kwa hiyari, kutoa elimu ya BIMA YA AFYA na uchangiaji wa damu.
  • Kwa watakao fika muda uliotangazwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, kila mmoja atapewa T-Shirt moja bure.
  • Michezo na burudani mbalimbali vitapamba uzinduzi huo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI INATEKELEZA MPANGO KAZI WA BLUE PRINT ILI KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI

Wadau wote kupitia vyama vyao waitwa kuleta mapendekezo ili kuboresha sekta zao ikiwa Serikali ipo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *