SERIKALI HAITAMVUMILIA MKANDARASI YEYOTE ATAKAYECHELEWESHA MIRADI YA NISHATI

  • Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amesema Serikali haitavumilia mkandarasi yeyote atakayechelewesha Miradi ya Nishati nchini.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI AKIWASHA UMEME WA REA
Naibu waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akiwasha rasmi umeme katika kijiji cha Ibaga Shule katika Wilaya ya Mkalama mkoani Singida. Mhe. Subira alifanya hayo alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA.
  • Mgalu amesema hayo wakati wa  ziara yake katika Wilaya ya Mkalama mkoani Singida ambapo aliwasha rasmi umeme katika kijiji cha Ibaga Shuleni, Ibaga center na Nkinto Ikurui pamoja na kukagua shughuli za utekelezaji wa mradi wa REA  II katika kijiji cha Nkinto Kinyantungu.
  • REA II wilayani Mkalama ilichelewa kukamilika kutokana na kampuni ya ukandarasi  ya Spencon iliyokuwa akitekeleza mradi huo kushindwa kufanya kazi hiyo kwa kiwango kinachotakiwa hivyo kuilazimu Serikali kusitisha mkataba wake na kuipatia kampuni nyingine ya ukandarasi ya JV Emec.
REA 3
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akikagua mashine ya kukamua mafuta ya alizeti. Mashine hiyo imeanza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa mara baada ya huduma ya umeme kufika katika kijiji cha Ibaga Shule na kuungwa kwenye mashine hiyo. Mhe. Naibu Waziri alikuwa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA katika wilaya Mkalama mkoani Singida.
  • Katika vijiji hivyo jumla ya wateja 48 wamelipia huduma ya umeme, 30 kati yao wamekwishaunganishwa  , 18 wanaendelea kuunganishwa, lengo likiwa ni kuwafikia wanakijiji wote katika Wilaya hiyo watakaokidhi viwango vya kuunganishwa na huduma hiyo.
  • Katika hatua nyingine, Mhe. Subira aliwaagiza mameneja wanaosimamia wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA kutoa taarifa mapema endapo hawaridhiswi na kasi ya wakandarasi ili Serikali iweze kuchukuwa hatua za haraka.
UMEME WA REA KWA KILA
Naibu waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akikagua usambaji wa umeme katika baadhi ya mitaaa ya kijiji cha Ibaga Center katika Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, baada ya umeme wa REA kufika kijijini hapo.

 

  • Aidha Serikali haitavumilia meneja yeyote atakayeshindwa kusimamia majukumu yake ikiwemo kumsimamia mkandarasi  anayetekeleza Miradi ya REA ili kukamilika kwa wakati na kupata matokeo chanya kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa jumla.
  • Alisema usimamizi wenye kuleta matokeo chanya ndiyo itakuwa kipimo cha utendaji kazi wa mameneja hao katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuunganisha vijiji vyote nchini na huduma ya umeme ifikapo mwaka 2021.
  • “Mameneja ninyi ndiyo mnakuwepo maeneno ya mradi wakati wote, mnafahamu kasi ya utendaji kazi wa mkandarasi na viwango, mkiona kama mkandarasi anasuasua hawezi kazi toeni taarifa mapema ili kazi hiyo apewe mwingine, Hatutakubali kurudisha nyuma, wananchi wanahitaji huduma ya umeme na fedha za kutekeleza hilo zipo!”, Alisisitiza Mgalu .
  • Aliagiza wakandarasi wote kuhakikisha wanakuwa na yadi za vifaa na miundombunu mbalimbali, kurahisisha  utekelezaji wa mradi husika.
  • Naibu waziri aliendelea kusisitiza kuwa ni marufuku  mkandarasi kuagiza Vifaa na miundombunu ya kutekeleza mradi wa REA  nje ya nchi, wakati vifaa hivyo vinapatikana hapa nchini.

 

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mama Mzazi wa Mama Janeth Magufuli (Juliana Stephano Kidaso) katika eneo la Kigongo Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza

4 Maoni

  1. You actually make it seem really easy along with your presentation but I find this matter to
    be actually something which I believe I’d never understand.
    It kind of feels too complicated and extremely broad for me.
    I am looking ahead to your next put up, I’ll
    attempt to get the hold of it! Escape room

  2. Rattling great info can be found on web site..

  3. I couldn’t refrain from commenting. Exceptionally well written!

  4. This website was… how do I say it? Relevant!! Finally I have found something that helped me. Thank you!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *