Balozi wa Tanzania nchini China Balozi Mbelwa Kairiki akifanya mazungumzo na kiongozi wa Jimbo la Guangdong azungumzo ambayo yameipa Tanzania fursa ya kutoa wafanyabiashara wanaoweza kwenda nchini China kwenda kutangaza bidhaa za Tanzania

FURSA KWA WAFANYABIASHARA; Milango Imefunguliwa Kutangaza Bidhaa za Tanzania Kwenye Soko la China

Jimbo la Guangdong limeahidi kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kushiriki katika maonesho mbalimbali ya biashara yanayoandaliwa kwa ajili ya kutangaza bidhaa za Tanzania katika soko la China.

BALOZI WA TANZANIA NCHINI CHINA ALETA FURSA KWA WAFANYABIASHARA NCHINI
Balozi wa Tanzania chini China Balozi Mbelwa Kairuki akifanya mazungumzo na kiongozi wa selikali ya jimbo la Guangdong Ndugu Zheng Jianlong

Ahadi hiyo imetolewa na kiongozi wa Serikali ya Jimbo hilo Ndugu Zheng Jianlong alipokutana na Balozi wa Tanzania nchini humo, Balozi Mbelwa Kairuki.

Ad
BALOZI KAIRUKI NA KIONGOZI WA JIMBO LA GUANGDONG
Baada ya mazungumzo yenye tija, Balozi Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na kiongozi wa jimbo la Guangdong Ndugu Zheng Jianlong.

Hii ni fursa kwa wafanyabiashara nchini kwenda kutangaza bidhaa za ndani za kilimo, madini na utalii ili kuweza kupata wawekezaji na soko bora na la uhakika kutoka nchi hiyo.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Uzinduzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya UCSAF Dodoma: Kuimarisha Mawasiliano Vijijini

25 Aprili 2024, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *