Waziri Mkuu Kassim Majaliwa . katikati mwenye Tai nyekundu atembelea DEGE ECO- VILLAGE mradi wa ubia kati ya Shirika la hifadhi ya Jamii NSSF na Azimiao wa Nyumba 7,4460 zilizopo Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam .kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF Balozi Ali Siwa.na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Azimiao. Mohammed Iqbal. Waziri Mkuu ametembelea mradi huo

Naagiza Wakurugenzi Wakuu wa NSSF, AZIMIO, Kamishna TRA wakutane – WAZIRI MKUU MAJALIWA

  • Waziri MkuuKassim Majaliwa ametembelea mradi wa nyumba unaojengwa kwa ubia kati Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kampuni ya Azimio Housing Estate Limited katika eneo la Dege Beach Kigamboni na kutamka kuwa amesikitishwa na uharibifu wa mali na wizi unaendelea kwenye eneo hilo.
  • Amewaagiza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio na Mkurugenzi wa Mkuu kampuni ya Azimio Housing Estate Limited, Mohammed Iqbal wakutane na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere ili wajadiliane namna ya kudhibiti wizi na kuimarisha ulinzi.

SISI-NI-TANZANIA-MPYA---23

  • Waziri Mkuu alitembelea eneo la mradi huo jana jioni (Jumatatu, Novemba 12, 2018) ambapo baada ya kufika katika eneo ambalo linajengwa nyumba zaidi ya 7,000 alionesha kusikitishwa na uharibifu wa mali na wizi unaoendelea na kutoa maagizo kwa wahusika.
  • “Kuna mpango gani wa ulinzi wa mali hapa, mali zinaendelea kuibiwa, tutakuja kuanza ujenzi hapa na kukuta hakuna mali hata moja. Ulinzi lazima uimarishwe pande zote mbili za mradi huu eneo la ujenzi na eneo la kuhifadhia vifaa vya ujenzi.”
WAZIRI MKUU KASSIM MAJA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia Majengo ya DEGE ECO- VILLAGE mradi wa ubia kati ya Shirika la hifadhi ya Jamii NSSF na Azimiao wa Nyumba 7,4460 zilizopo Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam.
  • Kwa upande wakeMkurugenzi Mkuu wa NSSF, Erio alimuahidi Waziri Mkuu kwamba atahakikisha wanakutana na Kamishna wa TRA na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya AZIMIO ili kujadiliana na namna ya kuimarisha ulinzi na kutatua changamoto ya wizi wa mali unaoendelea katika eneo hilo.
  • Mkataba kati ya NSSF na Azimio Housing Estate Limited (AHEL) ulisainiwa mwaka 2012 na kuanzisha kampuni ya hodhi ya “Hifadhi Builders” ambapo AHEL ilikuwa na asilimia 55 na NSSF asilimia 45. Katika asilimia 55 za AHEL, asilimia 20 ni ardhi iliyotoa kwenye mradi na asilimia 35 angetakiwa kuweka fedha taslimu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa .
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa . katikati mwenye Tai nyekundu atembelea DEGE ECO- VILLAGE mradi wa ubia kati ya Shirika la hifadhi ya Jamii NSSF na Azimio wa Nyumba 7,460 zilizopo Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam .kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF .Wiliam Erio na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Azimio. Mohammed Iqbal. Waziri Mkuu ametembelea mradi huo.
  • Mradi ulihusisha ujenzi wa nyumba 7,460 ambapo jumla ya gharama za mradi zilikadiriwa kuwa Dola za Marekani 653,436,675 ambazo kati yake ujenzi ungegharimu Dola 544,530,562 wakati gharama za ardhi zingekuwa Dola 108,906,113. Kwa fedha za Tanzania mradi pamoja na ardhi ungegharimu sh. trilioni 1.5.
  • Hadi kufikia Juni 2018 NSSF walishailipa kampuni ya Hifadhi Builders Dola 133,838,662.2 kama mchango wake kwenye ujenzi wa mradi huo ambazo ni sawa na sh. bilioni 305.8 wakati kampuni ya Azimio ikitoa Dola 5,500,000 sawa na sh. Bilioni 12.6 tu.
Ad

Unaweza kuangalia pia

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimfariji Katibu wa NEC (Uchumi na Fedha) wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Frank Hawassi kufuatia kifo cha Mke wake Bi. Damaris Hawassi wakati alipowasili kushiriki msiba huo Miyuji Jijini Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *