Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyeshwa namna madini ya Tanzanite yanavyotambulika na kuwekwa kwenye madaraja yake na Mtaalam wa Madini Bw. Jaffar Ally Mohamed wakati alipotembelea Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mererani.

Nasisitiza Zingatia Afya ya Mfanyakazi – MAKAMU WA RAIS

  • Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan amewataka wamiliki wa migodi na viwanda vya kuchenjua madini nchini kuzingatia haki na usalama wa wafanyakazi wao.
SISI-NI-TANZANIA-MPYA---29
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyeshwa namna madini ya Tanzanite yanavyotambulika na kuwekwa kwenye madaraja yake na Mtaalam wa Madini Bw. Jaffar Ally Mohamed wakati alipotembelea Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mirerani.

 

  • Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachotengeneza madini ya Kinywe (Graphite), Mirerani Wilayani Simanjiro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki kabla ya kuweka jiwe la msingi wa ufunguzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachochenjua madini ya Kinywe (Graphite), Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
  • Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Manyara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Meneja wa Kampuni ya Godmwanga Gem Ltd Bw. Andrew Mbando (katikati) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti (kulia) wakati alipotembelea kiwanda kinachomilikiwa na Mzawa kwa asilimia ambayo inachenjua madini ya Kinywe (Graphite).
  • “Pamoja na kuwekeza kupata pesa na kutoa ajira, kulipa kodi ni muhimu kuzingatia afya ya mfanyakazi kwa kumlinda kwa kumpatia vifaa vya usalama kazini pamoja na haki zao” alisema Makamu wa Rais.

SISI-NI-TANZANIA-MPYA---25

  • Kiwanda cha Gomwanga Gem Ltd kinamilikiwa Mtanzania kwa asilimia 100%, kinazalisha tani 60 kwa siku na kimeajiri Watanzania 80 ambacho mpaka sasa kimezalisha tani 3730.
SISI-NI-TANZANIA-MPYA---26
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachochenjua madini ya Kinywe (Graphite), Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
  • Kwa upande mwingine Waziri wa Madini Mhe. Angella Kairuki amesema kwa sasa Serikali imeweka zuio la kusafirisha madini ghafi mpaka yaongwezewe thamani hivyo amempongeza mmiliki wa kiwanda hicho kwa kuitikia maelekezo ya Serikali.SISI-NI-TANZANIA-MPYA---31
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachochenjua madini ya Kinywe (Graphite), Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI ATEMBELEA DAR ES SALAAM ZOO, AVUTIWA NA WANYAMA WENGI WANAOFUGWA HUMO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *