- Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na watalaam wengine wa afya leo wamehitimisha utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mtwara -Ligula- kwa kuhudumia wagonjwa 1476.
Kati ya hao, upasuaji mkubwa umefanyika kwa wagonjwa 54 na mdogo kwa wagonjwa 81. Baadhi ya upasuaji mkubwa uliofanyika ni kutoa uvimbe kwenye mfuko wa uzazi, kutoa matezi ya koo na matezi ya nyama ya pua (mafindofindo, kutoa tezi dume pamojan na kutoa mtoto wa jicho.
-
Maeneo ambayo wataalam wa Muhimbili kwa kushirikiana na wataalam wa Hospitali ya Ligula wamehudumia ni magonjwa ya dharura, Radiolojia magonjwa ya ndani, afya ya kinywa na meno,watoto ,magonjwa ya pua,koo na masikio, magonjwa ya kike na uzazi pamoja na mfumo wa mkojo.
-
Utoaji wa huduma za afya umeenda sambamba na kuwajengea uwezo wataalam wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mtwara ili waweze kutoa huduma bora za afya na kupunguza rufaa za kwenda Muhimbili. Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Ligula Dkt. Lobikieki Kissambu amewashukuru wataalam wa Muhimbili kwa kutoa huduma za afya katika hospitali hiyo na kueleza kuwa hospitali hiyo ina Daktari Bingwa mmoja tu hivyo ujio wa watalaam hao umewawezesha wananchi kupata huduma za kibingwa.
-
Utoaji wa huduma za afya kwa njia ya mkoba ni sehemu ya mpango mkakati wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ya kuhakikisha inatembelea Hospitali za Rufaa za Mikoa nchini ili kushirikiana nao na kuwajengea uwezo katika kutoa huduma ili kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda