Wataalamu wa nishati kutoka nchi wanachama wa Eastern Africa Power Pool (EAPP), wakiwa katika picha ya pamoja, kabla ya kuanza mkutano wao uliojadili masuala mbalimbali kuhusu mifumo ya kusafirisha umeme iliyounganishwa katika nchi husika. Mkutano huo umefanyika Februari 20, 2019 mjini Entebbe, Uganda.

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA 26 KUHUSU MIFUMO YA USAFIRISHAJI UMEME

  • Kamishana wa Umeme na Nishati Mbadala, Mhandisi Innocent Luoga, kutoka Wizara ya Nishati, ameongoza timu ya wataalamu wa nishati kutoka Tanzania, kushiriki katika mkutano wa 26 wa Kamati Tendaji unaojadili mifumo ya kusafirisha umeme, iliyounganishwa katika nchi zilizopo Mashariki mwa Afrika (Eastern Africa Power Pool – EAPP)
Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala
Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala, Mhandisi Innocent Luoga, akiwa katika kikao hicho
  • Mkutano huo unaofanyika, Februari 20, katika mji wa Entebbe nchini Uganda, ni wa ngazi ya wataalamu kutoka nchi wanachama, ukiwa ni utangulizi wa mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri wa sekta husika unaotarajiwa kufanyika, Februari 21, 2019.
  • Miongoni mwa masuala yanayojadiliwa, ni pamoja na maboresho ya mkataba wa ushirikiano kwa nchi wanachama wa EAPP.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka (wa kwanza – kulia), akiwa katika kikao hicho
  • Aidha, mkutano unajadili masuala ya biashara ya kuuziana na kusafirisha umeme kupitia mifumo ya EAPP na SAPP (Southern Africa Power Pool)
  • Nchi wanachama wa EAPP ni Tanzania, Uganda, Kenya, Ethiopia, Libya, Sudan, Misri, Rwanda, DRC na Djibouti.
Mhandisi Christopher Bitesigirwe
Mhandisi Christopher Bitesigirwe kutoka Wizara ya Nishati (kushoto) na Mhandisi Meksesius Kalinga kutoka TANESCO (kulia), wakiwa katika kikao hicho
  • Mbali na Kamishna Luoga, wataalamu wengine wanaoshiriki mkutano huo kutoka Tanzania ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt. Tito Mwinuka, Mhandisi Christopher Bitesigirwe kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Meksesius Kalinga kutoka TANESCO pamoja na Mhandisi Pius Gaspar kutoka TANESCO.
TIMU YA WATAALAM
Timu ya wataalamu wa nishati kutoka Tanzania, inayoshiriki katika mkutano unaojadili kuhusu mifumo ya kusafirisha umeme iliyounganishwa katika nchi za Mashariki mwa Afrika (Eastern Africa Power Pool – EAPP), mjini Entebbe, Uganda. Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala, Mhandisi Innocent Luoga (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka (wa pili – kulia), Mhandisi Christopher Bitesigirwe kutoka Wizara ya Nishati (kulia), Mhandisi Meksesius Kalinga kutoka TANESCO (kushoto) pamoja na Mhandisi Pius Gaspar kutoka TANESCO (wa pili – kushoto).
  • Katika mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri hapo kesho, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu atamwakilisha Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
Ad

Unaweza kuangalia pia

TPDC YAOKOA TRILIONI 12.7 KUAGIZA MAFUTA NJE YA NCHI

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *