KIWANDA CHA RUAHA MILLING COMPANY MKOMBOZI KWA WAKULIMA WA ZAO LA MPUNGA NYANDA ZA JUU KUSINI

 • Kiwanda cha Ruaha milling company kuchakata mpunga kilichopo mkoani iringa kimetajwa kuwa mkombozi kwa wakulima wa zao la mpunga ambalo limekuwa likilimwa kwa wingi katika wilaya ya Iringa na mkoa wa mbeya.
 • Akiwa ametembelea kiwanda hicho naibu meya manispaa ya Iringa,Joseph Ryata alisema kuwa kiwanda hicho kimejengwa kwa kiwango cha kimataifa ambacho kitasaidia kukuza kipato cha wakulima wa zao hilo.
KIWANDA
kiwanda cha Ruaha milling
 • “Kwa kweli jamani niseme ukweli kiwanda hiki ni moja ya viwanda bora sana hapa nchini ambavyo vinachakata mpunga kuwa mchele ukiangalia uwekezaji wake utagundua kuwa Ruaha milling company kinakuja kuwa mkombozi kwa wakulima wetu” alisema Ryata
 • Ryata aliwataka wakulima wa zao la mpunga kulima kwa wingi zao hilo kwa kuwa kiwanda cha Ruaha milling company kinahitaji kiwango kikubwa cha zao hilo ili kufanya kazi kwa uhakika hivyo wakulima jukumu lenu ni kulima kwa wingi na kwa ubora unaotakiwa.
KIWANDA
Naibu meya manispaa ya Iringa kupitia chama chama mapinduzi (CCM),Joseph Ryata akiwa na mkurugenzi wa kiwanda cha Ruaha milling company Atanas Kipeto wakiwa katika kiwanda hicho cha kuchakata mpunga kuwa mchele
 • “Naombeni nitoe rai kwa wakulima kulima kwa wingi zao hili kwa kuwa kiwanda hichi kinahitaji kuwa na tani nyingi za zao hilo la mpunga ili kuhakikisha kiwanda hicho kinafanya kazi kwa ufanisi unaotakiwa” alisema Ryata
 • Ryata alisema kuwa kiwanda hicho kimekuwa mkombozi kwa kuwa kinaongeza thamani ya zao hilo na kuongeza kipato kwa wakulima wa nyanda za juu kusini kwa kuanzisha kuwa na vifungashio ambavyo vinatoka katika kiwanda hicho.
 • “Kiwanda hichi kinafanya kila kitu na kinatenga chenyewe kulinga na ubora wa mchele wenyewe hivyo wakulima mnatakiwa kuwa na amani huku mkilima kilimo hicho kwa ubora unaotakiwa” alisema Ryata
Screenshot 2019-05-04 at 16.25.19
Mkurugenzi wa kiwanda cha Ruaha milling company Atanas Kipeto akiwa katika kiwanda hicho
 • Aidha Ryata alisema kuwa serikali inatakiwa kuendelea kuwaunga mkono wawekezaji wazawa kwa kuwa ndio wanafanya kazi ipasavyo kwa kutoa faida inayotakiwa kwa taifa.
 • Kwa upande wake mkurugenzi wa kiwanda cha Ruaha milling company,Atanas Kipeto alisema kuwa lengo la kujenga kiwanda hicho ni kuhakikisha anakuza thamani ya zao la mpunga na kukuza maisha ya wakulima ambao wamekuwa wakinyonywa na madalali.
KIWANDA
Naibu meya manispaa ya Iringa kupitia chama chama mapinduzi (CCM),Joseph Ryata akiwa na mkurugenzi wa kiwanda cha Ruaha milling company Atanas Kipeto akiwa na wadau wengine waliofika katika kiwanda hicho
 • “Mimi nimejenga kiwanda hiki kwa lengo tu la kuwapa thamini yao wakulima wa zao la mpunga ambao wamekuwa wakilima kwa taabu lakini hawapati ile faida au matunda yanayotakiwa kwa kununua bei nzuri ambayo inafaida kwa wakulima” alisema Kipeto
 • Kipeto aliongeza kuwa amekuwa akinunua zao la mpunga kwa kilo tofauti na wafanyabiashara wengine wanaonunua kwa gunia ambao kwa asilimia kubwa wamekuwa wakiwanyonya wakulima kwa kununua kwa kujaza lumbesa.
 • “Kununua kwa zao kwa kilo ni kuongeza thamani ya mazao kwa wakulima na ndio njia pekee ya kuacha kuwanyonya wakulima ambao ndio mara nyingi wamekuwa ngazi ya wafanyabiashara kutajirika” alisema kipeto
Ad

Unaweza kuangalia pia

KILA MTANZANIA ANAWEZA KUWEKEZA, TUMIENI FURSA ZILIZOPO – WAZIRI KAIRUKI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe. Angellah Kairuki …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *