TUONGEZE JUHUDI KATIKA VITA DHIDI YA MALARIA – RAIS MSTAAFU DKT. KIKWETE

 • Rais Mstaafu, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, katika nafasi yake kama mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End malaria Council) alialikwa kuwa mgeni rasmi katika kikao cha 20 cha mawaziri wa afya wa shirikisho la kiuchumi la nchi za Afrika magharibi – ECOWAS.
 • Kikao hicho kiliendeshwa chini ya chombo maalum cha afya cha ECOWAS kinachojulikana kama WAHO – (West African Health organization).
jk
Rais Mstaafu, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza  katika kikao cha 20 cha mawaziri wa afya wa shirikisho la kiuchumi la nchi za Afrika magharibi – ECOWAS.
 • Mkutano huu ni mwendelezo wa kikao cha kikazi ambacho Mhe. Kikwete aliendesha Addis Ababa mwezi wa pili mwaka huu alipokutana na wakuu wa taasisi za kikanda za kiuchumi na sasa anaendelea kuongea na mawaziri wa afya katika kanda hizo.
 • Akimkaribisha kuongea katika kikao hicho Prof. Stanley Okolo, Mkurugenzi mkuu wa WAHO, alimtambulisha Mhe. Kikwete kuwa ni mkereketwa wa masuala ya afya na mpiganaji katika azma ya kutokomeza malaria.
JK
Rais Mstaafu, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye ni mgeni rasmi   katika kikao cha 20 cha mawaziri wa afya wa shirikisho la kiuchumi la nchi za Afrika magharibi – ECOWAS, akiwa na viongozi wengeni meza kuu.
 • Kwani akiwa kama Rais wa Tanzania aliweza kuanzisha chombo cha viongozi wakuu wa Afrika wanaopambana na malaria ijulikanayo kama African Leaders Malaria Alliance (ALMA) ambacho kinaendelea kufanya kazi vizuri barani Afrika. Kwamba hata baada ya kustaafu Urais bado anayaendeleza mapambano hayo kwa kupitia taasisi ya kutokomeza malaria ambapo yeye ni mjumbe.
 • Taasisi ya kutokomeza malaria imeanzishwa na Bill gates na Ray Chambers na ina jumla ya wajumbe kumi na moja. Mhe. Kikwete alikutana na mawaziri hao kwa nia ya kwanza kuwaelezea waheshimiwa uwepo wa taasisi ya kutokomeza malaria, pia kuwasisitizia kuhusu umuhimu wa kuongeza nguvu katika vita dhidi ya malaria.
 • Katika Hotuba yake Mhe. Kikwete alielezea kuhusu tatizo la malaria duniani na azma ya Taasisi ya Kutokoeza Malaria kuhakikisha kuwa malaria inatoweka duniani kote.
JK
Rais Mstaafu, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza  katika kikao cha 20 cha mawaziri wa afya wa shirikisho la kiuchumi la nchi za Afrika magharibi – ECOWAS.
 • Mhe. Kikwete alisema kuwa pamoja na mafanikio mazuri yaliyopatikana wakati ya mwaka 2000 hadi 2015 ambapo malengo ya millenia ya kupunguza wagonjwa navifo vya malaria yalitimia, report ya malaria ya mwaka 2018 inaonesha kuwa mafanikio hayo yamesimama na kwamba katika mwaka 2017, Asilimia 90 ya wagonjwa na vifo vya malaria vya dunia nzima vilitokea Afrika.
 • Report hiyo pia imebainisha kuwa nchi 11 zinabeba asilimia 80 ya wagonjwa na vifo vya malaria. Ukiachia India nchi nyingine kumi zipo Africa ambazo ni Nigeria, Burkina Faso, Ghana, Niger, Mali, Cameroon, DRC, Mozambique, Uganda na Tanzania; na tano kati ya hizi zipo Afrika Magharibi. Nchi za ECOWAS bado zilibeba karibia nusu ya wagonjwa na vifo vya malaria vya dunia. Pamoja na kuwa hizi nchi kumi zinabeba asilimia kubwa ya malaria katika Afrika, hali ya malaria pia si nzuri katika nchi nyinginezo.
JK-1
Rais Mstaafu, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza  katika kikao cha 20 cha mawaziri wa afya wa shirikisho la kiuchumi la nchi za Afrika magharibi – ECOWAS.
 • Malaria ni ugonjwa ambao unaweza kutokomezwa kabisa hapa duniani, alielezea Mhe. Kikwete. Marekani ilitokomeza malaria mwaka 1956, China ambayo nayo ilikuwa na tatizo kubwa la malaria, katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo haijakuwa na mgonjwa hata mmoja wa malaria na hapo Africa magharibi nchi ya Cabo Verde ipo katika mwelekeo wa kuondokana na malaria wakati Gambia na kaskazini mwa Senegal nao wapo kwenye hatua nzuri.
 • Hivyo ni vyema tukajifunza pia kutoka kwao. Mheshimiwa Kikwete alisisitiza kuwa ni lazima juhudi za dhati ziwekwe ikiwa ni pamoja na uongozi wa juu wa serikali na wakuu wa Nchi kuwa mstari wa mbele katika mapambano.
 • Uongozi thabiti wa program za malaria, ushirikiano katika kanda zetu, ili kuondokana na ugonjwa huu ambao sio tu ni tatizo la kiafya bali ni tatizo la kimaendeleo na ni lazima kila sekta nayo ijue kuwa inayojukumu katika vita hivi dhidi ya malaria.
Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *