SERIKALI KUONDOA VIKWAZO VINAVYOATHIRI UWEKEZAJI NCHINI

  • Waziri wa Nchini Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji  Angellah Kairuki amebainisha mkakati maalum wa serikali kupitia utekelezaji wa BLUE PRINT wenye lengo la kuondoa vikwazo na changamoto zinazozuia ukuaji wa uwekezaji na urahisi wa kufanya biashara nchini.
  • Mkakati huo unapendekeza,pamoja na mambo mengine,marekebisho ya sheria mbalimbali,kuondoa urasimu na uratibu mzuri wa Mamlaka za Udhibiti bila kuleta usumbufu kwa Wawekezaji.
AN
Balozi wa Uingereza Nchini Bi Sarah Cooke akizungumza katika mkutano wa pamoja kati ya Serikali na Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka Uingereza
  • Kairuki ameyasema hayo jana katika Hotel ya Coral Beach,Dar es salaam wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Serikali na Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka Uingereza (British Business Group) kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili wawekezaji hao na kuahidi kuzitatua kwa hatua mbalimbali kwa kushirikiana na Taasisi za serikali ili kuifanya Tanzania sehemu nzuri ya uwekezaji.
AN
Waziri wa Nchini Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Mh Angellah Kairuki akizungumza katika mkutano wa pamoja kati ya Serikali na Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka Uingereza
  • Aidha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira  Anthony Mavunde amewashukuru Wawekezaji hao kwa kuendelea kutengeneza nafasi za Ajira kwa Watanzania kupitia Uwekezaji wao ambapo takribani Watanzania 300,000 wameajiriwa kupitia uwekezaji uliofanywa na Kampuni za Kutoka Uingereza nchini lakini pia amewataka wawekezaji hao kuzingatia sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini na Sheria ya Uratibu wa Ajira kwa wageni wakati wa uendeshaji wa shughuli zao hapa nchini.
AN
Waziri wa Nchini Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Mh Angellah Kairuki mkutano wa pamoja kati ya Serikali na Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka Uingereza,kushoto kwakwe ni Balazo wa Uingereza Nchini Bi Sarah Cooke
  • Akitoa salamu za Shukrani,Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kukubali wito wa kukutana na wawekezaji wao ili kusikiliza changamoto zao na kuahidi kuwa bega kwa bega na serikali katika kusaidia utekelezaji wa mkakati wa kuondoa vikwazo katika uwekezaji nchini Tanzania.
AN
Waziri wa Nchini Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Mh Angellah Kairuki akiwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI KAIRUKI AWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe. Angellah Kairuki …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *