- Kituo cha Television cha Hainan nchini China kimeingia makubaliano na Ubalozi wa Tanzania Beijing kutengeneza kipindi maalum cha kutangaza bidhaa za Tanzania, utamaduni, vyakula na utalii katika soko la China ambapo Kipindi hicho kitatengenezwa Mwezi Julai na kurushwa mwezi Novemba 2019
- Makubaliano hayo yamefikiwa Beijing katika mkutano wa Balozi wa Tanzania nchini humo,Mbelwa Kairuki na Mkurugenzi na Mtengenezaji wa Kipindi cha Travel Channel cha Hainan Television Bi Xie Xiao na timu yake. Bi Xiao ameeleza kwamba Televisheni hiyo ina watazamaji milioni 200 nchini China
Ad